Wimbo 15
Hatimaye—Uzima Bila Mwisho!
1. Waweza kuwazia,
Watu wawe pamoja?
Na huzuni, hakuna.
Hatima amani!
(Korasi)
2. Watu na hayawani,
Hawataumizana.
Kutakuwa chakula.
Wote watakula.
(Korasi)
3. Siku hizo wazee,
Watakuwa vijana.
Bila shida, hapana
Machozi na hofu.
(Korasi)
4. Furaha, paradiso
Na kutukuza Mungu.
Kila siku ’tasema
“Asante” E Mungu!
(KORASI)
Imba kwa furaha.
Waweza kuwapo.
Siku hiyo useme:
‘Uzima milele!’