Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • tr sura 16 kur. 140-150
  • Desturi Zinazopendwa na Watu Wengi Zinazomchukiza Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Desturi Zinazopendwa na Watu Wengi Zinazomchukiza Mungu
  • Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MATUMIZI YA MSALABA
  • SANAMU ZA KIDINI NA PICHA
  • KUHESHIMU WANADAMU NA VYAMA
  • EASTER NA KRISMAS
  • 22. (a) Jinsi gani Wagalatia 5:9 imepasa kuongoza nia yetu kuelekea Krismas? (b) Ni kwa sababu gani nzuri Wakristo huepuka mwadhimisho? 22 Hakuna kuepa: Krismas ni ya asili ya kipagani. Tukijua jambo hili imetupasa uliangalia onyo la mtume Paulo juu ya kuchanganya kweli na uongo. Yeye anasema kwamba hata “chachu kidogo huchachua donge zima.” (Wagalatia 5:9) Alikaripia baadhi ya Wakristo wa karne ya kwanza kwa kuadhimisha siku ambazo zilikuwa zimeadhimishwa chini ya sheria ya Musa lakini ambazo Mungu alikuwa amezifuta kwa Wakristo. (Wagalatia 4:10, 11) Jinsi ni jambo la muhimu zaidi sana kwa Wakristo wa kweli leo kuepuka mwadhimisho ambao haukuamriwa kamwe na Mungu, ambao asili yake ni katika Babeli wa kipagani, na ambao kwa uongo unachukua jina la Kristo! JAMBO LILILO BORA ZAIDI KULIKO MAADHIMISHO YA KIPAGANI
  • Itikadi na Desturi Ambazo Hazimpendezi Mungu
    Mungu Anataka Tufanye Nini?
  • Sikukuu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Je, Sherehe Zote Zinampendeza Mungu?
    Jinsi ya Kudumu Katika Upendo wa Mungu
  • Sherehe Ambazo Zinamchukiza Mungu
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
Pata Habari Zaidi
Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
tr sura 16 kur. 140-150

Sura ya 16

Desturi Zinazopendwa na Watu Wengi Zinazomchukiza Mungu

1. Kwa kutafuta kumpendeza Mungu, je! tunapata au tunapoteza?

SISI TUNACHO kila kitu kinachofaa kupata na bila kitu cha thamani ya kweli kupoteza kwa kutafuta kumpendeza Mungu katika mambo yote. Kwake yeye mtunga zaburi husema: “Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele.” (Zaburi 16:11) Walakini, Shetani Ibilisi hujaribu kugeuza watu mbali na ibada ya kweli na kuwaelekeza katika njia zimchukizazo Yehova Mungu. Mojawapo wa njia azitumiazo kutimiza hili ni mazoea ya desturi zinazopendwa na watu wengi ambazo ni kinyume cha mafundisho ya Biblia.

2. Jambo gani huamua kama desturi inayopendwa na watu wengi ni mbaya?

2 Si desturi zote zinazopendwa na watu wengi ni mbaya. Lakini zinamchukiza Mungu ikiwa zina shina katika dini ya uongo au ikiwa zinapingana na kanuni za Biblia katika njia fulani nyingine. (Mathayo 15:6) Kwa kupendeza, karibu desturi zote zinazopendwa na watu wengi ambazo zimesalia mpaka leo hii ni zile za aina ya kidini. Kwa kuwa tumekwisha kuona kwamba dini ya kilimwengu imegeuka kutoka kwa kawaida ya ibada ya kweli ya Biblia, isitushangaze kuona, kwamba nyingi za desturi zake zina msingi juu ya mazoea ya kipagani ya kidini.

3. (a) Ni onyo gani ambalo Yehova aliwapa watu wake juu ya desturi za kipagani za kidini? (b) Tunawezaje kusaidiwa kutumia shauri linalopatikana katika Warumi 12:2?

3 Katika kuwaonya Waisraeli juu ya desturi za kidini za mataifa yaliyowazunguka, Yehova aliwaambia watu wake kwamba isingewapasa wajifunze “njia ya mataifa hata kidogo.” (Yeremia 10:2, NW) Hili lilikuwa onyo la upendo, kwa sababu desturi hizo za kipagani zilikuwa na msingi juu ya uongo, zikimsingizia Mungu na kusudi lake. Mara nyingi desturi hizo zilikuwa na matokeo mabaya juu ya maadili ya wale waliozizoea. Kwa sababu inayofanana Biblia inatushauri sisi leo: “Mwache kufuatishwa kwa mtindo wa taratibu hii ya mambo, bali mgeuzwe kwa kukaza nia zenu, mpate kujithibitishia wenyewe mapenzi ya Mungu yaliyo mema na yenye kukubalika na makamilifu.” (Warumi 12:2, NW) Tamaa ya unyofu wa moyo kumpendeza Yehova Mungu itatusaidia sisi kufanya hivyo.

MATUMIZI YA MSALABA

4. Kitabu The Catholic Encyclopedia kinakubali nini juu ya msalaba?

4 Watu wengi waendao kanisani huvaa msalaba, au huwa na msalaba mdogo ulio na Yesu amepigiliwa msalabani nyumbani, na misalaba hupatikana katika majengo mengi ya kanisa. Je! wewe uliwahi kujua kwamba kweli msalaba ulikuwa na asili ya kipagani? Mambo ya hakika huonyesha jambo hilo, badala ya kuwa mfano wa pekee wa Kikristo, msalaba ulitumiwa kwa karne nyingi kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. Jambo hili linakubaliwa na The Catholic Encyclopedia (chapa ya mwaka wa 1908, Vol. IV, ukurasa wa 517):

“Ishara ya msalaba, ikionyeshwa katika umbo lake rahisi sana kwa kukingamanishwa kwa mistari miwili katika njia ya kukingama, hutangulia sana wakati wa mwanzo wa Ukristo katika Mashariki na Magharibi pia. Inarudi nyuma kwa kipindi cha mbali sana cha ustaarabu wa kibinadamu.”

5. Kitabu The Ancient Church kinasema nini juu ya asili ya kipagani ya msalaba?

5 Kikionyesha asili ya kidini ya kipagani ya msalaba, kitabu The Ancient Church kilichotungwa na padre W. D. Killen (chapa ya mwaka wa 1859, ukurasa wa 316 kinasema:

“Tangu zamani za kale zilizo mbali zaidi msalaba uli-heshimiwa katika Misri na Sham ; uliheshimiwa kwa kulingana na Wabuddha wa Mashariki; . . . karibu na mwanzo wa wakati wetu, wapagani walizoea kufanya ishara ya msalaba juu ya kipaji cha uso katika kuadhimisha kwa baadhi ya siri zao takatifu.”

6. Msalaba ulianzia wapi, na ulikuwa mfano wa mungu gani?

6 Na kuonyesha zaidi uhusiano wake na dini ya Kibabeli, W. E. Vine, katika An Expository Dictionary of New Testament Words (Vol. 1, ukurasa wa 256), husema kwamba msalaba “ulikuwa na asili yake katika Ukaldayo [Babeli] wa zamani, na ulitumika kama mfano wa mungu Tamuzi (ukiwa katika umbo la Tau ya siri [au T], herufi ya kwanza ya jina lake).”

7. (a) Kupatana na kitabu cha Biblia, cha Matendo, je! Yesu aliuawa penye msalaba wenye maboriti mawili? (b) Jinsi gani waandikaji wa zamani wa Kigiriki walitumia neno ambalo linatafsiriwa “msalaba” katika tafsiri fulani za Biblia?

7 Lakini je! Yesu hakuuawa penye msalaba wenye maboriti mawili? Biblia inaonyesha kwamba sivyo. Katika Matendo 5:30 na 10:39, tunaambiwa kwamba Yesu alifia penye “mti.” Hapa neno “mti” linatafsiri neno la Kigiriki la xylon (au xulon). Kuhusu neno hili na neno stauros, lililotafsiriwa “cross” (msalaba) katika tafsiri nyingine, The Companion Bible inasema penye ukurasa wa 186 katika “Appendixes”:

“Homer [mtunga mashairi wa zamani wa Kigiriki] hutumia neno stavros juu ya mti wa kawaida, au kipande kimoja cha mbao. Na hii ndiyo maana na matumizi ya neno katika maandishi yote bora ya zamani ya Wagiriki. Halimaanishi kamwe vipande viwili vya mbao vilivyowekwa kwa kukingama juu ya kimoja na kinglne katika pembe ye yote, ball sikuzote ni juu ya kipande kimoja peke yake. Ndiyo matumizi ya neno xulon [au xylon,, maana yake ni mbao] kuhusiana na jinsi ya mauti ya Bwana wetu, . . . Basi ushuhuda ni kamili, kwamba Bwana aliuawa penye mti ulionyoka, na si penye vipande viwili vya mbao vilivyowekwa kwa mkingamo wo wote.”

8. Matumizi ya msalaba yalianza lini miongoni mwa wale wajidaio kuwa, Wakristo? Na kwa nini walikubali ishara ya kipagani?

8 Akionyesha jinsi gani na wakati gani matumizi ya namna hiyo ya msalaba yalivyoanza miongoni mwa wale wajidaio kuwa Wakristo, W. E. Vine, katika kitabu chake, husema:

“Karibu katikati ya karne ya tatu A.D. ama makanisa yalikuwa yameondoka, ama yalikuwa [yamefanya mwigo uliopotoshwa mafundisho fulani ya dini ya imani ya Kikristo. Ili kuongeza sifa ya taratibu ya makanisa yenye kukufuru wapagani walipokewa katika makanisa bila wongofu kwa njia ya imani, na hasa waliruhusiwa kutunza ishara zao za kipagani na mifano. Kwa hiyo Tau au T, . . . ikiwa na kipande kilichokingama kimeshushwa, ilikubaliwa kusimama badala ya msalaba wa Kristo.”—Vol. 1, ukurasa wa 256.

9. (a) Je! ni jambo la kawaida kupenda chombo kilichotumiwa kumwua mpenzi? (b) Ikiwa mtu amekuwa akituniia msalaba, ni uamuzi gani ambao lazima afanye? Jambo gani litamsaidia katika kufanya uamuzi mzuri?

9 Siyo jambo la kawaida kupenda na kuabudu chombo kilichotumiwa kwa kumwua mtu fulani tumpendaye. Ni nani ambaye angefikiri kubusu bastola ambayo ilikuwa imetumiwa kwa kumwua mpenzi, au juu ya kuivaa shingoni mwa mtu? Kwa kuwa hivyo, na msalaba ukiwa umethibitishwa kuwa mfano wa kipagani wa kidini, watu ambao wamevaa kitu cha namna hiyo au walikuwa wanayo misalaba midogo nyumbani mwao, wakidhani kwamba jambo hili lilimheshimu Mungu na Mwanawe Yesu Kristo, wanakabiliwa na uamuzi wa muhimu. Je! wataendelea kuitumia? Je! hata wataitunza? Upendo wa kweli na tamaa ya kumpendeza Mungu katika mambo yote utawasaidia katika kufanya uamuzi mzuri.—Kumbukumbu la Torati 7:26.

SANAMU ZA KIDINI NA PICHA

10. (a) Ni umbali gani nyuma matumizi ya sanamu za kidini, mahali patakatifu na picha huanzia? (b) Kuhusu jambo hili, ni maswali gani ambayo yanastahili tuyaangalie?

10 Tangu wakati wa Misri ya zamani na Babeli, matumizi ya sanamu za kidini, mahali patakatifu na picha katika nyumba vimependwa na watu wengi. Vitu hivi vimependwa na watu waliosadiki kwamba vingewaletea usalama na baraka nyumbani mwao. Lakini je! Yehova anapendezwa na mazoea haya? Je! yeye anawakubali wale ambao hutazamia vita vya ibada vionekanavyo badala ya kuweka tumaini kamili katika yeye, Mungu wa kweli na aliye hai?

11. (a) Je! Mungu aliwaruhusu Waisraeli wa zamani kutumia sanamu za kidini kama misaada kwa ibada? (b) Kwa nini Wakristo wa kwanza pia waliepuka matumizi ya sanamu?

11 Kuonyesha kutokupendezwa kwake katika sana-mu za kidini na misaada kwa ibada, Mungu alitoa sheria yake kwa Waisraeli akiwakataza matumizi yake. Tena, aliwaonya juu ya kutamani dhahabu na fedha juu ya sanamu walizozikuta miongoni mwa watu wakipagani. (Kutoka 20:4, 5; Kumbukumbu la, Torati 7:25) Je! Mungu alibadili nia yake kwa kuanzwa kwa Ukristo? La, kwa maana Biblia huonyesha kwamba Wakristo vilevile waliepuka matumizi ya sanamu. (Matendo 17:29) Kwa kufuata shauri la mtume Yohana “jilindeni nafsi zenu na sanamu,” walitembea “kwa imani, si kwa kuona.” Waliweka tumaini lao kamili katika Mungu asiyeonekana.—1 Yohana 5:21; 2 Wakorintho 5:7.

12. Sanamu za Kristo zilianzaje? Basi, je! Wakristo wa kwanza walikuwa na sanamu za mama wa Yesu?

12 Historia ya kilimwengu hukubaliana na hili. Kama M’Clintock and Strong’s Cyclopcedia (Vol. IV, ukurasa wa 503) hutuambia: “Sanamu hazikujulikana katika ibada ya Wakristo wa kwanza.” Kwa kuwa Wakristo wa kwanza walitunza nyumba zao bila kuwa na sanamu za kidini, sanamu za Kristo zilianzia wapi? Kitabu The History of the Christian Religion and Church, During the Three First Centuries (kilichotungwa na Dr. Augustus Neander) (Chapa ya pili, ya mwaka wa 1848, ukurasa wa 183) kinatuambia: “Wapagani, ambao, kama vile Alexander Severus [Mtawala wa Kirumi wa karne ya tatu C.E.], waliona jambo fulani la Kimungu katika Kristo, na madhehebu, yaliyochanganya mambo ya kipagani na Ukristo pamoja, walikuwa ndio wa kwanza waliofanya matumizi ya sanamu za Kristo.” Kwa kuwa hapana sanamu za Kristo zilizotumiwa na Wakristo wa kwanza, ni wazi pia kwamba hawakuwa na sanamu za Mariamu, mama wa Yesu.

13. (a) Jambo gani huamua kama sanamu ya mtu au ya mnyama iliyochorwa kwa mti, chuma na mawe au picha humchukiza Mungu? (b) Ni nini asili ya “nimbus” au duara ya mwangaza kuzunguka kichwa cha Yesu?

13 Je! hii maana yake ni kwamba ni kosa kuwa na kitu cho chote cha sanaa, kama vile picha au sanamu za mtu au za mnyama zilizochorwa kwa mti, chuma na mawe, katika nyumba? La, kwa maana pana tofau-ti baina ya vitu vya vivi hivi vya sanaa na vitu vya ibada ya kidini. Ni jambo gani linaloamua kwamba sanamu ya mtu au ya mnyama iliyochorwa au picha haipendezi kwa Mungu? Ni hili: je! inaheshimiwa sana au kuabudiwa, labda mishumaa au chakula huwekwa mbele yake, kama ilivyo katika nchi fulani? Je! inasingizia Biblia? Au je! inaonyesha mifano ya kipagani? Labda wewe umeona kwamba picha nyingine za Yesu Kristo zina duara ya mwangaza kuzunguka kichwa chake. Hii inaitwa “nimbus.” Ikiwa unatazama neno “nimbus” katika encyclopedia, utajifunza kwamba ilitumiwa na Wamisri wa zamani, Wagiriki na Warumi katika usanifu wao wa kipagani wa kidini. Duara ya mwangaza kuzunguka kichwa inaweza kufuatiwa kurudi nyuma mpaka kwenye ibada ya jua ya Kibabeli, na inaonekana ikiwa na mifano ya miungu ya Babeli.

14. Watumishi waaminifu wa Mungu zamani walifanya nini wakati walipokuta vitu vya uongo vya kidini vya namna hiyo miongoni mwao?

14 Je! sisi tunao uongozi kutoka zamani kuhusu jambo gani imetupasa kufanya ikiwa tunazikuta sanamu za kidini za namna hiyo na picha zikiwa miongoni mwetu? Naam, Yakobo mwaminifu alifanya nini wakati alipoiona miungu ya uongo miongoni mwa washiriki wa jamaa yake? Aliiondoa kabisa. (Mwanzo 35:2-4) Naye kijana Mfalme Yosia alifanya nini kama matokeo ya kuanza kutafuta Mungu wa kweli? Aliziondoa sanamu za kuchora katika Yuda, akizivunja-vunja vipande vipande. (2 Mambo ya Nyakati 34:3, 4) Lo! mifano mizuri ya bidii namna gani katika kumpa Yehova Mungu utukufu !—Zaburi 115: 1-8, 18.

KUHESHIMU WANADAMU NA VYAMA

15. (a) Je ! sikukuu zinazotoa heshima za kuabudu kwa viumbe zinapendeza kwa Mungu? (b) Sikukuu za kukumbuka “roho za wafu” ziko juu ya msingi gani wa fundisho la dini la uongo? Basi, ni kweli gani juu ya Siku ya Roho Zote?

15 Katika mahali pengi ni desturi kuweka siku ya kuheshimu “watakatifu,” au watu maarufu, waliokufa au walio hai. Je! jambo hili linapendeza kwa Mungu? Biblia inaonya juu ya kutoa heshima za kuahudu kwa viumbe, hivyo sikukuu zinazoelekea katika upande huo hazipatani na mapenzi ya Mungu. (Matendo 10:25, 26; 14:11-15; Warumi 1:25; Ufunuo 19: 10) Tena, sikukuu za kukumbuka “roho za wafu” kwa kweli msingi wake ni juu ya fundisho la dini la uongo la kutoweza kufa kwa roho ya kibinadamu. Basi isitushangaze kusoma katika Encyclopcedia Britannica (chapa ya mwaka wa 1946, Vol. 1, ukurasa wa 666), kwamba “imani fulani zenye kupendwa na watu wengi zinazohusiana na Siku ya Roho Zote zina asili ya kipagani.” Watu wapendao njia ya kweli ni waangalifu kwa kuepuka maadhimisho ya namna hiyo.

16. (a) Kuna ubaya gani na sikukuu au maadhimisho yanayoheshimu mataifa au vyama vya kilimwengu? (b) Jinsi gani Maandiko huonyesha ni mwendo gani imewapasa Wakristo kuuchukua?

16 Sikukuu nyingine au maadhimisho huheshimu na kutukuza mataifa au vyama vya kilimwengu. Hapa desturi baya ni kuyapa sifa matengenezo ya namna hiyo kwa faida ambayo kweli imepaswa kupewa kwa Mungu, au kuhesabia vyama vya namna hiyo uwezo wa kuokoa na kulinda katika njia ambayo kweli Mungu peke yake ndiye awezaye kufanya. (Yeremia 17:5-7) Hivyo, washiriki wa maadhimisho haya humsingizia Mungu. Wakristo wa kweli wataongozwa na kanuni ya kwamba haiwapasi kuwa “sehemu ya ulimwengu.| (Yohana 15:19, NW) Badala ya kuiga ulimwengu, wao wataacha “kufuatishwa kwa mtindo wa taratibu hii ya mambo.”—Warumi 12:2, NW.

17. (a) Wakati wa mwadhimisho wa ukumbusho wa siku ya kuzaliwa, ni nani ambaye hutukuzwa kama kitu cha kuvuta macho ya watu? (b) Ni watu gani peke yao ambao maadhimisho yao ya ukumbusho wa siku za kuzaliwa yanaripotiwa katika Biblia? (c) Wakristo wa kwanza walionaje maadhimisho ya ukumbusho wa siku ya kuzaliwa?

17 Desturi nyingine ambazo huenda zionekane hazina hatia kabisa zinaongoza katika upande ule ule kama desturi zilizotajwa hapo juu. Hivyo, ijapokuwa mwadhimisho wa ukumbusho wa siku za kuzaliwa huenda ukaonekana kuwa si wa muhimu, unatukuza kiumbe, kumfanya yeye kuwa kitu cha kuvuta macho ya watu badala ya Muumba. Imetupasa kukumbuka, pia, kwamba maadhimisho mawili peke yake ya ukumbusho wa siku za kuzaliwa yanayotajwa katika Biblia ni yale ya Farao wa Misri na Herode Antipa, watawala waliofuata dini ya uongo. (Mwanzo 40:20-22; Mathayo 14:6-10) Na namna gani juu ya Wakristo wa kwanza? Mwandikaji wa historia Neander husema: “Wazo la sikukuu ya ukumbusho wa siku ya kuzaliwa lilikuwa mbali na mawazo ya Wakristo wa kipindi hiki kwa jumla.” (Ukurasa wa 190) Wao waliepuka maadhimisho ya ukumbusho wa siku za kuzaliwa kama za asili ya kipagani. Wale ambao kwa moyo wanataka kumpendeza Mungu kwa hekima huepuka desturi zinazotukuza kiumbe cho chote au ambazo asili yake ni dini ya uongo.—Yohana 5:44.

EASTER NA KRISMAS

18. (a) Je! Wakristo wa kwanza waliadhlmisha Easter? (b) Ni nini asili ya desturi za Easter zinazopendwa na watu wengi? (c) Je! mwadhimisho wa Easter una uthibitisho wo wote katika Biblia?

18 Easter ndiyo sikukuu iliyo kubwa kupita zote ya Kristendomu, inayosemwa kufanywa katika ukumbusho wa kufufuka kwa Kristo kutoka kwa wafu. Lakini je! Kristo alitoa amri kwa kuadhimisha ufufuo wake? La, hakutoa amri. Vitabu vya historia vinatuambia kwamba Easter haikuadhimishwa na Wakristo wa kwanza na ya kwamba msingi wake ni juu ya mazoea ya zamani ya kipagani. The Encyclopcedia Britannica kinasema:

“Hakuna ishara ya kuadhimishwa kwa sikukuu ya Easter katika Agano Jipya. . . . Utakatifu wa nyakati za pekee ulikuwa wazo ambalo halikuwamo katika akili za Wakristo wa kwanza.”a

Dr. Alexander Hislop husema juu ya desturi za Easter:

“Desturi zinazopendwa na watu wengi ambazo zingali zinafuatana na kipindi cha mwadhimisho wake kuthibitisha sana ushuhuda wa historia juu ya tabia yake ya Kibabeli. Mikate midogo ya moto yenye rnsalaba ya Ijumaa Kuu ya mayai yaliyopakwa rangi ya Pasaka au Easter Sunday, ilikuwako katika kanuni za dini za Kikaldayo [Kibabeli] kama ilivyoko sasa.”b

Neno “Easter” linaloonekana mara moja katika Biblia ya Kiingereza ya King James katika Matendo 12:4 ni tafsiri yenye makosa ya neno la “passover.”c (sikukuu ya kupitwa). “Easter” halionekani mahali po pate katika Biblia ya Catholic Douay. Kwa hiyo, Easter, sikukuu iliyo kubwa kupita zote za Kristendomu, haithibitishwi hata kidogo na Biblia. Ni ya asili ya kipagani, na kwa hiyo inamchukiza Mungu.

19. (a) Je! Krismas iliadhimishwa na Wakristo wa kwanza? (b) Ni ukumbusho gani ambao Yesu aliwaagiza wafuasi wake kuadhimisha?

19 Namna gani juu ya Krismas? Kwa kuchunguza katika vitabu katika maktaba ya watu wote, utaona kwamba haikujulikana miongoni mwa Wakristo wa kwanza. Yesu aliwaagiza wafuasi wake kuadhimisha ukumbusho wa mauti yake, si ukumbusho wa kuzaliwa kwake. (1 Wakorintho 11:24-26) Chasema kitabu The Catholic Encyclopedia: “Krismas haikuwamo miongoni mwa sikukuu za kwanza za kanisa. . . . Ushuhuda wa kwanza wa sikukuu ni kutoka Misri.”d

20. (a) Jinsi gani mambo ya hakika huonyesha kwamba Yesu asingaliweza kuzaliwa wakati wa majira ya baridi sana? (b) Ni lini tarehe ya Desemba 25 ilipochaguliwa, na kwa nini tarehe hiyo?

20 Basi, namna gani juu ya tarehe ya Desemba 25, inayoadhimishwa na wengi kama siku ya kuzaliwa kwa Yesu. Biblia inaonyesha kwamba wakati huo wachungaji walikuwa wangali makondeni usiku. Kama vile Encyclopcedia Britannica (cha mwaka wa 1907, Vol. V, ukur. 611) kikubalivyo, wasingalikuwako makondeni wakati huo kwa sababu ni majira ya baridi sana na yenye mvua. (Luka 2:8-12) Kwa habari ya asili ya tarehe hiyo, The World Book Encyclopedia kinasema:

“Katika A.D. 354, Askofu Liberins wa Rumi aliwaamu- ru watu kuadhimisha siku ya Desemba 25. Labda alichagua tarehe hii kwa sababu watu wa Rumi walikwisha kuiadhimisha kama Sikukuu ya Saturn, wakiadhimisha siku ya kuzaliwa kwa jua.”e

21. Mambo ya hakika ya historia yanaonyesha nini kwa habari ya asili ya karibu desturi zote za Krismas?

21 Kwa kuwa tarehe ya Krismas ni ya asili ya kipagani, isionekane ajabu kwamba desturi za Krismas pia ni za asili ya kipagani. Ndivyo kitabu Encyclopedia of Religion and Ethics kituambiavyo:

“Karibu desturi zote za Krismas ambazo sasa ziko . . . si desturi za kweli za Kikristo, bali ni desturi za kipagani ambazo zimekubaliwa au kuvumiliwa na Kanisa. . . . Sikukuu ya Saturn katika Rumi iliweka kielelezo kwa zaidi ya desturi za shangwe za wakati wa Krismas.”f

Tena, The Encyclopedia Americana kinaonyesha kwamba miongoni mwa desturi zilizochukuliwa kutoka kwa karamu ya Kirumi ya sikukuu ya Saturn ilikuwa desturi ya “kutoa zawadi.”g

22. (a) Jinsi gani Wagalatia 5:9 imepasa kuongoza nia yetu kuelekea Krismas? (b) Ni kwa sababu gani nzuri Wakristo huepuka mwadhimisho?

22 Hakuna kuepa: Krismas ni ya asili ya kipagani. Tukijua jambo hili imetupasa uliangalia onyo la mtume Paulo juu ya kuchanganya kweli na uongo. Yeye anasema kwamba hata “chachu kidogo huchachua donge zima.” (Wagalatia 5:9) Alikaripia baadhi ya Wakristo wa karne ya kwanza kwa kuadhimisha siku ambazo zilikuwa zimeadhimishwa chini ya sheria ya Musa lakini ambazo Mungu alikuwa amezifuta kwa Wakristo. (Wagalatia 4:10, 11) Jinsi ni jambo la muhimu zaidi sana kwa Wakristo wa kweli leo kuepuka mwadhimisho ambao haukuamriwa kamwe na Mungu, ambao asili yake ni katika Babeli wa kipagani, na ambao kwa uongo unachukua jina la Kristo! JAMBO LILILO BORA ZAIDI KULIKO MAADHIMISHO YA KIPAGANI

23. Wakristo wa kweli wana jambo gani lililo bora sana kuliko “roho ya Krismas” ya mara moja kila mwaka?

23 Wakristo wa kweli wanalo jambo fulani

bora zaidi kuliko maadhimisho ya kipagani. Wao wanayo “matunda ya roho.” (Wagalatia 5:22, 23, NW) Matunda haya hufanyiza ukarimu ambao ni mzuri zaidi sana na wa kweli kuliko “roho ya Krismas” ambayo husitawi mara moja tu kila mwaka. Roho ya Mungu hufanyiza fadhili na kuwafikiria wengine ambako kwaweza kuonwa waziwazi kila siku ya kila mwaka. Jambo hili huwaongoza Wakristo kutoa, si kwa kutumaini kulipwa au kwa sababu wanalazimishwa kutoa, bali kwa sababu ya upendo wa kweli wa Kikristo.​—Luka 6:35, 36; Matendo 20:35.

24. (a) Ni wakati gani Wakristo wa kweli hutoa zawadi na kuwa na vipindi vya furaha vya kuwa pamoja? (b) Jinsi gani jambo hili ni bora kuliko jambo ambalo ulimwengu hufanya?

24 Wakristo wa kweli wanaweza kutoa zawadi na kuwa na vipindi vya furaha vya kuwa pamoja katika mwaka wote. (Luka 6:38) Si lazima wazazi wangojee ukumbusho wa siku za kuzaliwa au Krismas, bali wanaweza kuwaletea watoto wao zawadi kwa nyakati mbalimbali wakati wa mwaka. Jambo hili husaidia kukitia nguvu kifungo cha upendo baina ya wazazi na watoto. Tena, watoto hawatiwi moyo kuwa wasio na shukrani kwa wanadamu au kwa Mungu, kwa sababu ya kufikiri kwamba wanastahili kupokea zawadi katika siku fulani.—Wakolosai 3:14.

25. Kujifunza kweli juu ya desturi zinazopendwa na watu wengi hutuweka sisi huru na nini, na kwa kutumainia mradi gani?

25 Kujifunza kweli juu ya asili za kipagani za desturi zinazopendwa na watu wengi kwaweza kuleta matokeo ya ajabu ya kuwa huru. Hatuwi tena chini ya wajibu wa kuzifuata desturi ambazo zimeonekana kuwa mzigo kwa watu wa ulimwengu kwa fedha na kwa njia nyingine. Na zaidi sana, kujua kwetu kweli hutuweka sisi kuwa huru kufuatia mwendo ambao unapendeza kwa Yehova, ili tuweze kupata uzima wa milele katika taratibu yake mpya ya haki.—Yohana 8:32; Warumi 6:21, 22.

[Maelezo ya Chini]

a The Encyclopcedia Britannica, cha mwaka wa 1910, Vol. VIII, ukur. 828.

b The Two Babyions, kur. 107, 108.

c Tazama tafsiri za kisasa za Biblia za Matendo 12:4 au The Westminster Dictionary of the Bible, ukur. 145.

d The Catholic Encyclopedia, cha mwaka wa 1908, Vol. III, ukur. 724.

e The World Book Encyclopedia, cha mwaka wa 1966, Vol. VI, ukur. 416.

f Encyclopedia of Religion and Ethics, cha James Hastings, Vol. III kur. 608, 609.

g The Encyclopedia America, cha mwaka wa 1956, Vol. VI, ukur. 632.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki