Wimbo 175
Mbingu Zatangaza Utukufu wa Mungu
1. Mbingu zinamutukuza Yehova;
Kazi zake juu angani twaona.
Kucha kuchwa kwamusifu
Usiku na usiku fahari yake.
2. Sheria ya Yehova ni kamili,
Navyo vikumbusho vinahekimisha.
Maagizo ni furaha;
Na amuri zake zang’arisha macho.
3. Kumwogopa Yah ni kwa umilele.
Hukumu zake ni adili na kweli
Na dhahabu zaipita.
Kama asali, milele, ziko tamu.
4. Asante kwa sheria, vikumbusho;
Na kwa kuzishika twavuna thawabu.
Kazi na mawazo yetu
Yawe manyofu na kweli, yapendeze.