Wimbo 95
Tunda la Wema
1. Yehova Mwenyezi ni wa daima,
Yamufananisha sifa ya wema.
Kwa rehema alituma Mwanake
Wanyofu dhambi zao wazitubu.
2. Wafungua watu, wema wa Mungu
Katika Babeli yenye uovu.
Wazidisha nuru itumulike,
Mema na mabaya yapambanuke.
3. Basi na tuige wema wa Mungu;
Tulikuze tunda la roho yake.
Tuwe wakarimu, tutakasike;
Mungu na Yesu tuwatumaini.
4. Tuzidishe wema kwa njia gani?
Funzo, utumishi, na sala pia.
Pamoja na ndugu tukutanike,
Na hivyo kwa wema tukamilike.