Wimbo 207
Sisi Tu Mali ya Nani?
1. Wewe ni wa nani?
Wamutii nani?
Huyo umwinamiaye
Huyo ndiye Bwana wako.
Shida kuabudu
Miungu wawili,
Kuwapenda kikamili wote,
Mabwana wawili.
2. Wewe ni wa nani?
Utatii nani?
Kuna mwongo na wa kweli,
Chagua, ni juu yako.
Kaisari ndiye
Utii kabisa?
Au utii Mungu wa kweli
Umutumikie?
3. Mimi ni wa nani?
Yehova n’tatii.
Nitatumikia huyo
Nifanye nadhiri yangu.
Alininunua
Siabudu watu.
Nimekombolewa kwa Mwanaye;
Sigeuki tena.
4. Sisi ni wa Mungu
Hakuna mashaka.
Alitabiri umoja
Twaona zizini mwake.
Ni mafuta juu
Kichwa cha kuhani,
Twaona uzuri kukutana
Tufunzwe ukweli.