Wimbo 138
O Enda Pamoja na Mungu!
(Mika 6:8)
1. Enda na Mungu kiasi;
Zipende fadhili.
Ushike ukamilifu;
Na akupe nguvu.
Ukishika kweli yake,
Usidanganyike;
Mungu na akuongoze,
Sawa na kitoto.
2. Enda na Mungu kisafi;
Dhambi usifanye.
Ili ukomae sana
Uwe na kibali.
Usafi, wema wowote
Uutafakari,
Na ili uvumilie,
Tumaini Mungu.
3. Enda naye kwa imani,
Nawe utapata
Utawa, na kuridhika,
Ni faida kubwa.
Enda naye; sifa zake
Uwe wamwimbia.
Ufalme wake ’taleta
Shangwe kubwa sana.