Wimbo 213
Kufanya Kazi kwa Umoja
1. Na tutende kwa umoja.
Na tusijitegemee.
Upatano, nia moja
Zaleta amani.
Umoja baraka.
Ndivyo ilivyo.
Tusiringie karama,
Na tusiwe na kiburi.
Kiasi pia upendo,
Na tusifu Mungu.
2. Uadui, wivu umo
Ulimwenguni wa chuki.
Tunatafuta amani.
Inaburudisha.
Inaburudisha.
Kama umande.
Kukosana huwa pia;
Si wakamilifu sisi!
Na tupatane haraka.
Umoja udumu.
3. Na kazini kila siku,
Na tuonyeshe umoja.
Ni bora na wapendeza.
Tutunze umoja.
Ndiyo, tuutunze,
Kwani ni bora
Umoja una thawabu
—Hivyo twakaa na Mungu.
Amerejeza amani,
Kwake Bwana yetu.