Wimbo 92
Hubiri kwa Ujasiri
1. Watumishi wake Yehova,
Lazima wawe nazo nguvu.
Twapata ushujaa ndani
Ya Neno hata mahubirini.
Neno la Mungu hupa nguvu,
Na nia ya kuendelea,
Na kuwa washikamanifu.
Kama mitume tuwe ’jasiri.
2. Tunaamini kwa mioyo
Neno la Mungu ni la kweli,
Sisi hatuogopi watu;
Twaamini japo wachache tu.
Tukaze fikira kazini
Tueneze neno la Mungu.
Kwa kuhubiri kijasiri,
Yehova ni Rafiki milele.
3. Uwasaidie wanyonge,
Ili waseme kijasiri.
Usiwasahau wachanga;
Wasaidie wapate nguvu.
Wafariji wauguao,
Wote wategemee Mungu.
Ataitawala dunia
Wanadamu wamwimbie sifa.