Wimbo 71
Zishike Sana Habari Njema!
1. Ijapo saa ya mwisho,
Na tuwe imara.
Tuifanye kazi ngumu,
Kwa nguvu za Mungu.
Ukweli unaangaza,
Kuna kazi nyingi.
Kazi yetu si ya bure
’Tapata furaha.
2. Tumai’ la ufufuo
Lahuisha moyo,
Huimarisha imani.
Laleta furaha.
Uwe imara, hodari;
Kwenda ushindini.
Twataka kuziamini
Ahadi za Mungu.
3. Tujitahidipo sana
Tupate muradi,
Tutafute ushirika
Mwema ujengao.
“Habari” za Paradiso
Zakaza tumai’.
Asante kwa Mungu wetu
Kwa Yesu Bwanetu.