Wimbo 9
Baraka ya Yehova Hutajirisha
1. Yehova hupa baraka nyingi.
Tunapotumikia.
Furaha ni nyingi tukipanda
Mioyoni maneno.
2. Ijapo mengi mateso, chuki,
Na yote twahimili,
Rehema za Mungu twaziona,
Twakuta majaribu.
3. Tukiyatimiza tuwezayo,
Kufanya mambo mema,
Mungu ambaye ni mwaminifu,
Atapendezwa nasi.
4. Basi, sisi tuwe na bidii.
Baraka tutapata!
Na fadhili zake ’tafunua;
Haongezi huzuni.