Wimbo Na. 8
Mlo wa Jioni wa Bwana
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova Baba wa mbinguni,
Leo siku ya pekee!
Mwezi wa Nisani kaonyesha nguvu,
Upendo, haki, hekima.
Mwana-Kondoo aliliwa,
Israeli wakatoka.
Ba’daye Bwana kamwaga damu yake,
Na kutimiza unabii.
2. Mbele zako tumekutana,
Tukiwa kondoo zako.
Tukusifu wewe kwa upendo wako,
Tuheshimu jina lako.
Tuzingatie Ukumbusho,
Moyoni, na akilini.
Tufuate hatua za Kristo Yesu,
Kisha uzima wa milele.
(Ona pia Luka 22:14-20; 1 Kor. 11:23-26.)