Wimbo Na. 131
Yehova Huokoa
1. Mungu wetu uliye hai, Yehova.
Kazi zako kuu, dunia na mbingu.
Hakuna Mungu kama wewe hasha—hakuna.
Wakujue wewe.
(KORASI)
Yehova huokoa wa’minifu.
Wamwone kuwa Mungu wa nguvu nyingi.
Kwa bidii na ujasiri sisi sote,
Twatangaza jina kuu lake Yehova.
2. Japo kuna kifo, nakutegemea,
“Yehova unipe, ujasiri, nguvu.”
Toka hekalu lako, usikie, ‘Nifiche,
Niokoe, Mungu.’
(KORASI)
Yehova huokoa wa’minifu.
Wamwone kuwa Mungu wa nguvu nyingi.
Kwa bidii na ujasiri sisi sote,
Twatangaza jina kuu lake Yehova.
3. Utakaponguruma kutoka juu.
Maadui wako, waingiwe hofu.
Wakutumikiao, wafurahi. Wajue
U mwokozi wetu.
(KORASI)
Yehova huokoa wa’minifu.
Wamwone kuwa Mungu wa nguvu nyingi.
Kwa bidii na ujasiri sisi sote,
Twatangaza jina kuu lake Yehova.
(Ona pia Zab. 18:1, 2; 144:1, 2.)