Wimbo Na. 150
Tumejitoa Kutumikia
Makala Iliyochapishwa
Ee Yehova unajua
jinsi ya kutupa shangwe.
Waandaa njia nyingi,
sisi tukutumikie.
(KORASI)
Yehova, twafanya,
yote twezayo.
Kwenye uhitaji, twaenda.
Tumejitoa.
Kazi nyingi kotekote.
Tunaenda, kujitoa.
Twawajali, watu wote.
msaada tunawapa.
(KORASI)
Yehova, twafanya,
yote twezayo.
Kwenye uhitaji, twaenda.
Tumejitoa.
Twajifunza lugha mpya.
Na ujenzi twashiriki.
Twajaribu mbinu mpya,
Tufunze habari njema.
(KORASI)
Yehova, twafanya,
yote twezayo.
Kwenye uhitaji, twaenda.
Tumejitoa.
(Ona pia Yoh. 4:35; Mdo. 2:8; Rom. 10:14.)