Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr17 Mei kur. 1-2
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
  • Vichwa vidogo
  • MEI 1-7
  • MEI 8-​14
  • MEI 15-​21
  • MEI 22-​28
  • MEI 29–JUNI 4
Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
mwbr17 Mei kur. 1-2

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

MEI 1-7

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 32-​34

it-1 105 ¶2

Anathothi

Yeremia alikuwa mzaliwa wa Anathothi lakini alikuwa ‘nabii ambaye hakuheshimiwa’ na watu wa nyumbani kwake, ambao walitishia kumuua kwa sababu ya kuzungumza ujumbe wa kweli kutoka kwa Yehova. (Yer 1:1; 11:​21-23; 29:27) Matokeo ni kwamba Yehova alitabiri jiji hilo lingepatwa na msiba, na jambo hilo lilitokea Wababiloni walipovamia nchi hiyo. (Yer 11:​21-23) Kabla ya kuanguka kwa Yerusalemu, Yeremia alitumia haki yake ya kisheria kununua shamba lililokuwa Anathothi kutoka kwa binamu yake. Kwa kununua shamba hilo Yeremia alitoa ishara kwamba Israeli wangerudi kutoka uhamishoni. (Yer 32:​7-9) Kikundi cha kwanza kilichorudi kutoka uhamishoni ambacho kiliongozwa na Zerubabeli kilikuwa na wanaume 128 kutoka Anathothi; na Anathothi ilikuwa mojawapo ya miji ambayo ilimilikiwa tena baada ya watu kurudi kutoka uhamishoni, na hivyo kutimiza unabii wa Yeremia.​—Ezra 2:23; Neh 7:27; 11:32.

MEI 8-​14

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 35-​38

it-2 1228 ¶3

Sedekia

Ukweli unaoonyesha kwamba Sedekia alikuwa kiongozi dhaifu sana ulionekana wazi wakati wakuu walipomwomba amuue Yeremia kwa madai kwamba alikuwa anawakatisha tamaa watu waliozingirwa, Sedekia alisema hivi: “Tazama! Yuko mikononi mwenu. Kwa maana hakuna jambo lolote ambalo mfalme anaweza kuwazuia ninyi.” Hata hivyo, baadaye Sedekia alikubali maombi ya Ebed-meleki ya kumwokoa Yeremia na aliagiza kwamba Ebed-meleki achukue wanaume 30 pamoja naye ili wamsaidie. Baadaye, Sedekia alikuwa tena na mazungumzo ya siri na Yeremia. Alimhakikishia nabii huyo kwamba hangemuua wala kumkabidhi mikononi mwa watu waliokuwa wakitafuta kumuua. Lakini Sedekia aliogopa kwamba Wayahudi waliokuwa wamejiunga na Wakaldayo wangelipiza kisasi, na hivyo hakutii onyo lililoongozwa na roho la Yeremia ambaye alimshauri ajisalimishe kwa wakuu wa Babiloni. Alionyesha woga zaidi alipomwomba Yeremia asifunue mazungumzo yao ya siri kwa wakuu aliowatilia shaka.​—Yer 38:​1-28.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 759

Warekabu

Yehova alipendezwa na utii wa heshima walioonyesha. Utii wao usioyumba-yumba kumwelekea baba yao wa kidunia ulitofautiana sana na ukosefu wa utii ambao Wayudea walionyesha kumwelekea Muumba wao. (Yer 35:​12-16) Mungu aliwapa Warekabu ahadi hii yenye thawabu: “Hatakatiliwa mbali kutoka kwa Yonadabu mtu wa kusimama mbele zangu sikuzote.”​—Yer 35:19.

MEI 15-​21

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 39-​43

it-2 1228 ¶4

Sedekia

Kuanguka kwa Yerusalemu. Hatimaye (607 K.W.K.), “katika mwaka wa kumi na moja wa Sedekia, katika mwezi wa nne, katika siku ya tisa ya mwezi huo,” Yerusalemu lilibomolewa. Wakati wa usiku Sedekia na wanajeshi wake walitoroka. Walipokamatwa kwenye jangwa tambarare la Yeriko, Sedekia alipelekwa kwa Nebukadneza ambaye alikuwa Ribla. Wana wa Sedekia waliuawa mbele ya macho yake. Kwa kuwa Sedekia alikuwa na umri wa miaka 32 wakati huo, bila shaka wavulana wake walikuwa na umri mdogo sana. Baada ya kushuhudia vifo vya wanawe, Sedekia alipofushwa macho, akafungwa pingu za shaba, na kupelekwa Babiloni ambako alifungwa gerezani mpaka alipokufa.​—2Fa 25:​2-7; Yer 39:​2-7; 44:30; 52:​6-11; linganisha na Yer 24:​8-10; Eze 12:​11-16; 21:​25-27.

it-2 482

Nebuzaradani

Nebuzaradani, akiwa amepewa maagizo na Nebukadneza, alimwachilia Yeremia na kuzungumza naye kwa fadhili, akamruhusu Yeremia achague mahali ambapo angependa kwenda, akamlinda na kumpa chakula na zawadi. Nebuzaradani pia alikuwa msemaji wa Mfalme wa Babiloni alipomchagua Gedalia kuwa gavana wa watu ambao hawakupelekwa uhamishoni. (2Fal 25:22; Yer 39:​11-14; 40:​1-7; 41:10) Miaka mitano hivi baadaye, mwaka 602 K.W.K., Nebuzaradani aliwachukua Wayahudi wengine na kuwapeleka uhamishoni, hasa wale waliokuwa wamekimbilia maeneo mengine.​—Yer 52:30.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 463 ¶4

Mfuatano wa Matukio

Yerusalemu lilizingirwa kwa mara ya mwisho mwaka wa 9 wa utawala wa Sedekia (609 K.W.K), na jiji hilo lilianguka katika mwaka wa 11 wa utawala wake (607 K.W.K), huo ulikuwa mwaka wa 19 wa utawala halisi wa Nebukadneza (tukihesabu tangu alipokuwa Mfalme mwaka wa 625 K.W.K). (2Fa 25:​1-8) Katika mwezi wa tano wa mwaka huo (mwezi wa Abi, ambao ni sawa na sehemu za miezi ya Julai na Agosti) jiji lilichomwa moto, kuta zikaangushwa, na watu wengi walipelekwa uhamishoni. Hata hivyo, baadhi “ya watu wa hali ya chini wa nchi,” waliruhusiwa kubaki, na waliendelea kuishi hapo mpaka Gedalia, kiongozi aliyechaguliwa na Nebukadneza alipouawa, nao wakakimbilia Misri na kuliacha Yuda likiwa ukiwa kabisa. (2Fa 25:​9-12, 22-26) Huo ulikuwa mwezi wa saba, Ethanimu (au Tishri, ambao ni sawa na sehemu za miezi ya Septemba na Oktoba). Hivyo hesabu ya miaka 70 ya ukiwa lazima ilianza Oktoba 1 hivi, mwaka wa 607 K.W.K., na kuisha mwaka wa 537 K.W.K. Kufikia mwezi wa saba wa mwaka huo wa mwisho, Wayahudi wa kwanza kutoka uhamishoni walifika Yuda, miaka 70 tangu kuanza kwa ukiwa kamili wa nchi hiyo.​—2Nya 36:​21-23; Ezra 3:1.

MEI 22-​28

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 430

Kemoshi

Nabii Yeremia akitabiri msiba kwa Moabu, alionyesha kwamba mungu wao mkuu Kemoshi pamoja na makuhani wake na wakuu wake wangepelekwa uhamishoni. Wamoabu wangemwaibikia mungu wao kwa kuwa ni dhaifu, kama vile Waisraeli wa ufalme wa makabila kumi walivyoona aibu kwa sababu ya Betheli, labda kwa sababu jiji hilo lilihusianishwa na ibada ya ndama.​—Yer 48:​7, 13, 46.

it-2 422 ¶2

Moabu

Utimizo sahihi wa unabii kuhusu Moabu hauwezi kupingwa. Karne nyingi zilizopita Wamoabu walikoma kuwa kikundi cha watu. (Yer 48:42) Leo, majiji yanayoonwa kuwa yalikuwa ya Moabu, kama vile Nebo, Heshboni, Aroeri, Beth-gamuli na Baal-meoni yamebaki yakiwa magofu. Sehemu nyingine nyingi hazijulikani leo.

MEI 29–JUNI 4

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 49-​50

it-1 54

Adui

Watu wa Mungu walipokosa kuwa waaminifu aliwaruhusu adui zao wawavamie na kuwashinda. (Zb 89:42; Law 1:5, 7, 10, 17; 2:17; 4:12) Hata hivyo, adui hao walifikia mkataa usiofaa kutokana na ushindi huo, wakijisifu wenyewe na kuitukuza miungu yao au walihisi kwamba hawangetozwa hesabu kwa jinsi walivyowatendea watu wa Yehova. (Kum 32:27; Yer 50:7) Kwa hiyo, Yehova alilazimika kuwanyenyekeza adui hao waliojisifu na kujitukuza (Isa 1:24; 26:11; 59:18; Nah 1:2); na alifanya hivyo kwa sababu ya jina lake takatifu.​—Isa 64:2; Eze 36:​21-24.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 94 ¶6

Waamoni

Inawezekana Waamoni walianza kukaa kwenye eneo la kabila la Gadi baada ya watu wa ufalme wa kaskazini wa Israeli kupelekwa uhamishoni na Tiglath-pileseri wa Tatu akishirikiana na mmoja wa warithi wake (2Fa 15:29; 17:6), kwa kuwa awali Waamoni hao walikuwa wameshindwa vitani walipopigana na Waisraeli waliokuwa wakiongozwa na Yeftha. (Linganisha Zb 83:​4-8.) Hivyo, kupitia ujumbe wa kinabii ambao Yehova aliwapa kupitia Yeremia, Waamoni walikaripiwa kwa kuwapokonya Wagadi urithi wao na walionywa kuhusu kuja kwa ukiwa dhidi ya Amoni na mungu wake Malkamu (Milkomu). (Yer 49:​1-5) Waamoni walitenda uovu zaidi kwa kuwatuma wanyang’anyi ili waitese Yuda ambayo ilikuwa ikitawaliwa na Mfalme Yehoyakimu katika miaka ya mwisho mwisho ya ufalme wa Yuda.​—2Fa 24:​2, 3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki