Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr17 Septemba uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
  • Vichwa vidogo
  • SEPTEMBA 4-10
  • SEPTEMBA 11-​17
  • SEPTEMBA 18-24
  • SEPTEMBA 25–OKTOBA 1
Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
mwbr17 Septemba uku. 1

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

SEPTEMBA 4-10

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | EZEKIELI 42-45

it-2 1082 ¶2

Hekalu

Maono ya Ezekieli ya Hekalu. Mwaka wa 593 K.W.K., katika mwaka wa 14 baada ya uharibifu wa Yerusalemu na hekalu la Sulemani lililokuwa jijini humo, nabii Ezekieli ambaye pia alikuwa kuhani, alisafirishwa katika maono hadi kwenye kilele cha mlima, na kuonyeshwa hekalu kubwa la Yehova. (Eze 40:1, 2) Ili kuwaaibisha na kuwafanya Wayahudi waliorudi kutoka uhamishoni watubu, na pia bila shaka ili kuwafariji waaminifu, Ezekieli aliagizwa aisimulie “nyumba ya Israeli” kila kitu alichoona. (Eze 40:4; 43:10, 11) Maono hayo yalikazia uangalifu vipimo vilivyochukuliwa. Vipimo vilivyotumiwa ni vya “utete” (urefu wa utete, futi 10.2) na “mkono” (urefu wa mkono, sentimita 51.8). (Eze 40:5) Uangalifu ulioelekezwa kwenye vipimo hivyo umewafanya watu fulani waamini kwamba maono hayo ya hekalu yalipaswa kutumiwa katika hekalu lililojengwa baadaye na Zerubabeli baada ya uhamisho. Hata hivyo, hakuna uthibitisho kamili wa madai hayo.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 467 ¶4

Jina

Kwa kuwa Israeli walikuwa watu wa jina la Mungu, kushindwa kwao kuishi kulingana na amri zake za uadilifu kulikuwa kukufuru au kutia unajisi jina la Mungu. (Eze 43:8; Amo 2:7) Pia, kwa kuwa kukosa uaminifu kwa Waisraeli kulifanya Mungu awape adhabu, hilo liliwapa nafasi watu wa mataifa mengine kusema kwa njia isiyo na heshima kuhusu jina la Mungu. (Linganisha Zb 74:10, 18; Isa 52:5.) Kwa kuwa mataifa hayo yalishindwa kutambua kwamba adhabu hiyo ilitoka kwa Yehova, yalifikiri kimakosa kwamba Israeli lilianguka kwa sababu Yehova alishindwa kuwalinda watu wake. Ili kuondolea jina lake suto, Yehova alichukua hatua kwa ajili ya jina lake na kuwarudisha mabaki ya Israeli kwenye nchi yao.—Eze 36:22-24.

it-2 140

Haki

Hivyo, sikuzote Yehova amedai kwa haki kwamba wale wanaotamani kupata kibali chake wajifunze viwango vyake vya haki na kuvifuata. (Isa 1:17, 18; 10:1, 2; Yer 7:5-7; 21:12; 22:3, 4; Eze 45:9, 10; Amo 5:15; Mik 3:9-12; 6:8; Zek 7:9-12) Kama Mungu, hawapaswi kuwa na upendeleo, kwa sababu upendeleo ni ukosefu wa haki na unavunja sheria yake ya upendo. (Yak 2:1-9) Hata hivyo, kutekelezwa kwa haki kupatana na kiwango cha Mungu si mzigo; furaha ya wanadamu inategemea kufuata kiwango hicho. (Zb 106:3; linganisha Isa 56:1, 2.) Blackstone, mwanasheria maarufu wa Uingereza, alikubaliana na ukweli huo: “[Mungu] ameunganisha sheria za haki zinazodumu milele na furaha ya kila mwanadamu, hivi kwamba hakuna anayeweza kuwa na furaha bila kuwepo kwa haki; na ikiwa haki itatendwa kwa wakati unaofaa, bila shaka furaha itapatikana.”​—Chadman’s Cyclopedia of Law, 1912, Buku la 1, uk. 88.

SEPTEMBA 11-​17

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | EZEKIELI 46-​48

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 1001

Mwana wa Binadamu

Katika Maandiko ya Kiebrania, maneno hayo yanapatikana mara nyingi zaidi katika kitabu cha Ezekieli, ambapo Mungu anamwita nabii huyo “mwana wa binadamu” zaidi ya mara 90. (Eze 2:1, 3, 6, 8) Inaonekana kwamba maneno hayo yanatumiwa ili kukazia kwamba nabii huyo ni mwanadamu tu, na hivyo kuonyesha wazi kabisa tofauti iliyopo kati ya msemaji huyo wa kibinadamu na Chanzo cha ujumbe wake, yaani, Mungu Aliye Juu Zaidi. Nabii Danieli anaitwa hivyo pia kwenye Danieli 8:17.

SEPTEMBA 18-24

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | DANIELI 1-3

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 382

Meshaki

Kuna sababu tatu ambazo huenda ziliwafanya waamue kwamba chakula kitamu cha mfalme ni chenye ‘kutia unajisi’: (1) Wababiloni walikula vyakula ambavyo si safi kulingana na Sheria ya Musa; (2) hawakuwa waangalifu ili kuhakikisha kwamba wanyama waliochinjwa wameondolewa damu ifaavyo, na huenda wengine walinyongwa; (3) mara nyingi wapagani walitoa dhabihu ya wanyama hao kwa miungu yao kwanza, na hivyo waliona kula nyama hizo kuwa sehemu ya ibada yao kwa miungu hiyo.—Da 1:8; linganisha na 1Ko 10:18-20, 28.

SEPTEMBA 25–OKTOBA 1

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | DANIELI 4-6

Kutafuta Hazina za Kiroho

w88 10/1 30 ¶3-5

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Wakati yule Mwebrania mwenye kuitwa Danieli alipoletwa ndani hatimaye, mfalme alirudia kutaja toleo lake—kumvika Danieli kwa rangi ya zambarau, kumvalisha mkufu wa dhahabu, na kumfanya awe mtawala wa tatu katika ufalme ule. Nabii alijibu hivi kiheshima: “Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.”—Danieli 5:17.

Kwa hiyo Danieli hakuhitaji kuhongwa au kulipwa ndipo aandae fasiri ile. Mfalme angeweza kuweka zawadi zake au kumpa mtu mwingineye. Danieli angeandaa elezo, si ili apate thawabu, bali kwa sababu yeye alitiwa nguvu za kufanya hivyo na Yehova, yule Mungu wa kweli, ambaye hukumu yake ilikuwa ikining’inia juu ya Babuloni.

Kama vile sisi tunavyosoma kwenye Danieli 5:29, baada ya Danieli kuwa amesoma na kutafsiri maneno yale kama alivyosema angefanya, mfalme aliagiza kwamba thawabu zile zipewe kwa Danieli ingawaje. Danieli hakujivalisha nguo zile na mkufu ule. Alivalishwa kwa agizo la yule mtawala mwenye mamlaka kamili, Mfalme Belshaza. Lakini hiyo haihitilafiani na Danieli 5:17, ambapo nabii alielewesha wazi kwamba kusudio lake halikuwa la ubinafsi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki