Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb18 Januari uku. 8
  • Kwanza Fanya Amani na Ndugu Yako​—Jinsi Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwanza Fanya Amani na Ndugu Yako​—Jinsi Gani?
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Habari Zinazolingana
  • Jambo la Kufanya Unapoudhi Wengine
    Amkeni!—1996
  • Wewe Husuluhishaje Matatizo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Suluhisha kwa Upendo Hali ya Kutoelewana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
  • Msiwakwaze “Hawa Wadogo”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2021
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
mwb18 Januari uku. 8

MAISHA YA MKRISTO

Kwanza Fanya Amani na Ndugu Yako​—Jinsi Gani?

Mwanamume akiacha dhabihu yake kwenye madhabahu na kwenda kufanya amani na ndugu yake

Wazia kwamba unaishi Galilaya katika siku za Yesu. Umesafiri kwenda Yerusalemu ili kusherehekea Sherehe ya Vibanda. Jiji la Yerusalemu limejaa waabudu wenzako ambao wamekuja kutoka maeneo mbalimbali. Unataka kutoa toleo lako kwa Yehova. Kwa hiyo, unamvuta mbuzi wako na kujaribu kupita katika mitaa ya jiji hilo iliyojaa watu ukielekea hekaluni. Unapofika, hekalu limejaa watu wanaotaka kutoa dhabihu pia. Mwishowe, zamu yako inafika ya kuwakabidhi makuhani mbuzi wako. Papo hapo unakumbuka kwamba ndugu yako ana jambo fulani dhidi yako. Hujui yeye yuko wapi katika umati huo au katika jiji. Yesu anaeleza jambo unalopaswa kufanya. (Soma Mathayo 5:24.) Wewe na ndugu uliyemkosea mnaweza kufanya nini ili kufuatilia amani kama Yesu anavyotuagiza? Katika kila orodha iliyo hapa chini, tia alama kando ya jibu sahihi.

UNAPASWA . . .

  • kuzungumza na ndugu yako ikiwa tu unafikiri kwamba ana sababu nzuri za kukasirika

  • kujaribu kurekebisha kufikiri kwa ndugu yako ukihisi kwamba amekasirika bila sababu au analaumika kwa kiasi fulani kwa sababu ya tatizo hilo

  • kusikiliza kwa subira ndugu yako anapojieleza, na hata ikiwa huelewi kikamili, umwombe msamaha kwa unyoofu kwa kumwumiza hisia au kwa sababu ya matokeo yasiyotarajiwa ya matendo yako

NDUGU YAKO ANAPASWA . . .

  • kuwaambia wengine kutanikoni jinsi ulivyomkosea ili wamwunge mkono

  • kukuaibisha, kutaja makosa yote uliyofanya, na kudai ukubali umekosea

  • kutambua kwamba ulihitaji unyenyekevu na ujasiri ili kuongea naye, na akusamehe kwa hiari kutoka moyoni

Ingawa ibada yetu haihusishi dhabihu za wanyama, Yesu alikuwa akifundisha kuna uhusiano gani kati ya amani na ndugu yetu na ibada inayokubalika machoni pa Mungu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki