Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb18 Februari uku. 4
  • “Mheshimu Baba Yako na Mama Yako”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mheshimu Baba Yako na Mama Yako”
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Habari Zinazolingana
  • Kufurahisha Mioyo ya Wazazi Wako
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Heshimu Wanadamu Wa Namna Zote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Kuwaheshimu Wazazi Wetu Wazee-Wazee
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Inamaanisha Nini ‘Kumheshimu Baba Yako na Mama Yako’?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
mwb18 Februari uku. 4

MAISHA YA MKRISTO

“Mheshimu Baba Yako na Mama Yako”

Yesu alipokuwa duniani, alikazia amri hii: “Mheshimu baba yako na mama yako.” (Kut 20:12; Mt 15:4) Bila shaka, Yesu alikuwa na uhuru wa kusema kwa sababu ‘aliendelea kuwatii’ wazazi wake alipokuwa kijana. (Lu 2:51) Alipokuwa mtu mzima, alihakikisha kwamba mama yake angetunzwa baada ya kifo chake. —Yoh 19:26, 27.

Katika siku zetu pia, vijana Wakristo wanaowatii wazazi wao na kuzungumza nao kwa heshima wanawaonyesha staha. Kwa kweli, amri ya kuwaheshimu wazazi inapaswa kuendelea kufuatwa milele. Hata wazazi wetu wanapozeeka, tunapaswa kuendelea kuwaheshimu na kufaidika kutokana na hekima yao. (Met 23:22) Pia, tunawaheshimu wazazi wetu waliozeeka kwa kuwatunza kihisia na kifedha inapohitajika. (1Ti 5:8) Iwe sisi ni watoto au watu wazima, kudumisha mawasiliano mazuri na wazazi wetu ni njia muhimu ya kuwaonyesha heshima.

TAZAMENI VIDEO YA VIBONZO KWENYE UBAO NINAWEZAJE KUZUNGUMZA NA WAZAZI WANGU? KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Kwa nini huenda ikawa vigumu kuzungumza na wazazi wako?

  • Unaweza kuwaonyeshaje wazazi wako heshima unapozungumza nao?

    Mvulana akiwaandikia barua wazazi wake, akizungumza na wazazi wake, na akicheza mpira wa miguu na baba yake
  • Unanufaikaje unapozungumza na wazazi wako? (Met 15:22)

    Wazazi wakimsaidia kijana wao kukabiliana na matatizo ya wakati ujao

    Kuzungumza na wazazi wako kunaweza kukusaidia kufanikiwa maishani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki