WIMBO NA. 20
Ulimtoa Mwana Wako Mpendwa
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova, Ee Baba,
Tu watenda-dhambi
Fidia imetupa
tumaini!
Twataka kufanya
yote tuwezayo
Wengine wajue,
wema wako wote.
(KORASI)
Mwanao mpendwa,
Ulitoa afe.
Tutaimba milele,
Kwa kutupa Mwana wako.
2. Fadhili, rehema,
Zatuvuta kwako.
Twasema asante,
na twathamini
kutoa Mwanao
kwa ajili yetu
uzima tupate
twashukuru sana.
(KORASI)
Mwanao mpendwa,
Ulitoa afe.
Tutaimba milele,
Kwa kutupa Mwana wako.
(UMALIZIO)
Yehova, Ee Baba, Tunakushukuru.
Twasema asante, kutoa Mwana wako.
(Ona pia Yoh. 3:16; 15:13.)