Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • th somo la 9 uku. 12
  • Kutumia Picha na Video Vizuri

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutumia Picha na Video Vizuri
  • Boresha Uwezo Wako wa Kusoma na Kufundisha
  • Habari Zinazolingana
  • Kutumia Vizuri Vielelezo
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Tumia Video Kufundisha
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Tumia Video Kuwafundisha Wanafunzi Wako wa Biblia
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2019
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Boresha Uwezo Wako wa Kusoma na Kufundisha
th somo la 9 uku. 12

SOMO LA 9

Kutumia Picha na Video Vizuri

Andiko lililotajwa

Mwanzo 15:5

MUHTASARI: Tumia picha na video ili kufanya mambo unayofundisha yawe wazi na yaeleweke kwa urahisi.

JINSI YA KUFANYA HIVYO:

  • Chagua vielelezo vitakavyoboresha ufundishaji wako. Unapotoa hotuba unaweza kutumia picha, michoro, ramani, mpangilio wa matukio, au vielelezo vingine vya aina hiyo ili kuonyesha mambo makuu wala si mambo madogo-madogo. Katika huduma unaweza pia kutumia video ili kutimiza kusudi hilo. Wasaidie wasikilizaji wako wakumbuke si tu vielelezo ulivyotumia bali jambo kuu lililofanya utumie vielelezo hivyo.

  • Hakikisha wasikilizaji wako wanaweza kuona vielelezo vyako. Kwa mfano, ikiwa utaonyesha picha jukwaani hakikisha ni kubwa vya kutosha ili wasikilizaji waweze kuiona.

    Dokezo linalofaa

    Muda mrefu kabla ya kutoa mgawo wako, hakikisha kwamba picha, video, au chochote ulichopanga kutumia kiko tayari.

KATIKA HUDUMA

Msaidie mwenye nyumba atafakari kuhusu picha iliyo katika chapisho, na umwombe atoe maelezo kuhusu anachoona. Muulize maswali ya ziada kadiri inavyohitajika ili kukazia mawazo makuu. Unapomwonyesha video, shika kifaa chako kwa njia ambayo anaweza kuona vizuri. Kwa kawaida, huhitaji kuzungumza unapoonyesha video.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki