Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr19 Februari uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
  • Vichwa vidogo
  • FEBRUARI 25–MACHI 3
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
mwbr19 Februari uku. 1

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

FEBRUARI 25–MACHI 3

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | WAROMA 9-11

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 1260 ¶2

Mwenye Wivu, Wivu

Bidii isiyoelekezwa kwa njia inayofaa. Mtu anaweza kuwa na bidii, au awe na wivu, wa kutimiza jambo fulani lakini wakati huohuo awe amekosea na awe anamkasirisha Mungu. Ilikuwa hivyo kwa Wayahudi wengi katika karne ya kwanza. Walifikiri kazi walizofanya chini ya Sheria ya Musa zingewafanya kuwa waadilifu. Lakini Paulo alionyesha kwamba bidii yao ilielekezwa kwa njia isiyofaa kwa sababu hawakuwa na ujuzi sahihi. Hivyo, hawakupata uadilifu wa kweli unaokuja kutoka kwa Mungu. Walipaswa kutambua kosa lao na kumgeukia Mungu kupitia Kristo ili wapate uadilifu na uhuru kutokana na hukumu ya Sheria ya Musa. (Ro 10:1-10) Sauli wa Tarso alikuwa mmoja kati yao. Alikuwa na bidii nyingi kupita kiasi katika dini ya Kiyahudi kufikia hatua ya “kulitesa sana kutaniko la Mungu na kuliangamiza.” Alikuwa akiishika Sheria kikamili akiamini alikuwa “mtu ambaye hakuwa na hatia.” (Gal 1:13, 14; Flp 3:6) Hata hivyo, wivu wake kwa ajili ya dini ya Kiyahudi ulikuwa umeelekezwa vibaya. Alikuwa na moyo mnyoofu, na hiyo ndiyo sababu Yehova alimwonyesha fadhili zisizostahiliwa kupitia Kristo na kumgeuza afuatie ibada ya kweli.—1Ti 1:12, 13.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki