WIMBO NA. 85
Karibishaneni
Makala Iliyochapishwa
1. Mwakaribishwa mikutanoni.
Mjifunze Neno la Mungu.
Linalotupa sote uhai;
Tunauthamini mwaliko wa Mungu.
2. Asante Mungu, kwa wachungaji,
Ndugu zetu watupendao.
Twawathamini, twawaheshimu
Na wengine pia twawakaribisha.
3. Enyi wanyo’fu, mwakaribishwa,
Kuipata njia ya kweli.
Mungu na Kristo, wametuvuta.
Tukaribishane kwa moyo mweupe.
(Ona pia Yoh. 6:44; Flp. 2:29; Ufu. 22:17.)