Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mrt makala 34
  • Je, Ugaidi Utakwisha?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Ugaidi Utakwisha?
  • Habari Zaidi
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mungu anahisije kuhusu ugaidi?
  • Chanzo halisi cha ugaidi
  • Mwisho wa ugaidi
  • Ugaidi Utakoma Karibuni!
    Amkeni!—2001
  • Hatimaye Amani Duniani!
    Amkeni!—2006
  • Historia Iliyojaa Umwagaji wa Damu
    Amkeni!—2006
  • Ukurasa wa Pili
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Habari Zaidi
mrt makala 34
Mzima-moto aokoa waokokaji katika majengo yaliyoporomoka.

Je, Ugaidi Utakwisha?

Ugaidi unapotokea, huenda ukajiuliza hivi: ‘Je, Mungu anajali? Kwa nini mambo haya yanatokea? Je, ugaidia utakwisha? Nitafanyaje kwa kuwa ninahisi wasiwasi mwingi?’ Biblia inatupatia majibu yanayoridhisha ya maswali hayo.

Mungu anahisije kuhusu ugaidi?

Mungu anachukia ukatili na ugaidi. (Zaburi 11:5; Methali 6:16, 17) Yesu ambaye ni mwakilishi wa Mungu, aliwakemea wanafunzi wake walipotenda kwa ukatili. (Mathayo 26:50-52) Ingawa baadhi ya watu hudai kutumia jina la Mungu wanapotenda kwa ukatili, Mungu haungi mkono matendo yao. Na hata hasikilizi sala zao.—Isaya 1:15.

Mungu anawajali watu wanaoteseka, na wote wanaoathiriwa na mashambulizi ya kigaidi. (Zaburi 31:7; 1 Petro 5:7) Pia, Biblia inasema kwamba Mungu atachukua hatua ya kukomesha ukatili.—Isaya 60:18.

Chanzo halisi cha ugaidi

Biblia inaeleza wazi sababu ya msingi inayofanya kuwe na ugaidi: “Mwanadamu amemtawala mwanadamu mwenzake kwa kumuumiza.” (Mhubiri 8:9) Katika historia yote, wanadamu wenye mamlaka wametenda kwa ugaidi ili kuwakandamiza wengine. Na matokeo ni kwamba wengine wametenda kwa njia hiyo pia ili kulipiza kisasi.—Mhubiri 7:7.

Mwisho wa ugaidi

Mungu ameahidi kwamba ataondoa wasiwasi na ukatili na kuleta amani duniani. (Isaya 32:18; Mika 4:3, 4) Ataondoa:

  • Mambo yanayosababisha ugaidi. Mungu ataondoa serikali za wanadamu na kusimamisha serikali yake itakayotawala ulimwenguni pote. Mtawala wa serikali hiyo, Yesu Kristo, atawatendea watu wote kwa haki, naye ataondoa ukandamizaji na ukatili. (Zaburi 72:2, 14) Katika utawala wake, hakuna yeyote atakayetenda kwa ugaidi. Watu “watafurahia kwelikweli wingi wa amani.”—Zaburi 37:10, 11.

  • Madhara yote yanayosababishwa na ugaidi. Mungu atawaponya watu walioathiriwa na ugaidi, iwe ni madhara ya kimwili au ya kihisia. (Isaya 65:17; Ufunuo 21:3, 4) Pia, ameahidi kwamba atawafufua watu waliokufa ili waishi tena katika dunia yenye amani.—Yohana 5:28, 29.

Biblia inataja sababu nzuri zinazotusaidia kuamini kwamba Mungu atachukua hatua hivi karibuni. Hata hivyo, huenda unajiuliza hivi, ‘Kwa nini Mungu bado hajachukua hatua ya kukomesha ugaidi?’ Ili upate jibu la swali hilo, tazama video Kwa Nini Mungu Anaruhusu Kuteseka?

a “Ugaidi” umefafanuliwa kuwa matumizi au vitisho vya kutumia nguvu na ukatili hasa kwa raia ili kutekeleza mabadiliko ya kisiasa, kidini au kijamii. Hata hivyo, huenda watu wasikubaliane na baadhi ya mambo yanayoweza kuonwa kuwa ni ugaidi.

Biblia huwasaidia watu kukabiliana na hali hiyo

Biblia inataja mambo haya mawili yanayoweza kukusaidia.

  • Sali kwa Mungu.—Wafilipi 4:6, 7.

  • Kazia fikira ujumbe wa Biblia kuhusu tumaini.—Waebrania 6:19.

Ili ujifunze mengi zaidi kuhusu mapendekezo yanayotegemea Biblia, soma makala “Jinsi ya Kudhibiti Wasiwasi.”

Mashahidi wa Yehova ambao wamevumilia vitendo vya ugaidi wamepata msaada pia kutoka kwa waamini wenzao. Ona mifano miwili inayofuata:

  • Maua ya ukumbusho yaliyowekwa nje ya shule iliyo Beslan, Urusi.

    Natalya na mwana wake mwenye umri wa miaka tisa anayeitwa Aslan, walikuwa katika shule iliyo huko Beslan, nchini Urusi, wakati ambapo magaidi wenye silaha kali waliingia kushambulia ghafla na kuwachukua mateka watu zaidi ya 1,000. Kwa kusikitisha, mamia ya watu walikufa hasa watoto wadogo kwa sababu ya mashambulizi hayo ya kigaidi. Ingawa Natalya na Aslan waliokoka lakini bado waliathiriwa sana na shambulizi hilo. Ona jambo lililowasaidia kukabiliana na hali hiyo.

  • Pablo na Sophie.

    Pablo na Sophie, Mwana wao alikufa wakati wa mashambulizi yaliyotokea katika majengo ya Twin Towers huko New York. Tazama video hii ili uone jambo lililowasaidia wao na wengine walioathiriwa na shambulizi hilo la ugaidi.

Biblia huwasaidia watu kubadili maisha

Watu wengi wamevunjika moyo kwa sababu ya ukosefu wa haki na ukandamizaji uliopo ulimwenguni. Huenda wakahisi kwamba ukatili na ugaidi ndiyo suluhisho pekee la matatizo. Je, watu hao wanaweza kubadilika? Jibu ni Ndiyo. Ili ujifunze jinsi ujumbe wa Biblia ulivyowasaidia baadhi ya watu kubadili maisha, soma makala “Je, Inawezekana Kuwa na Ulimwengu Usio na Ugaidi?”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki