WIMBO NA. 28
Kuwa Rafiki ya Yehova
Makala Iliyochapishwa
1. Nani rafikiyo?
Akaaye kwako?
Nani ambaye wamwamini?
Nani akujua?
Washikao Neno,
Wakuaminio,
Watenda haki na walio
washikamanifu.
2. Nani awezaye
kukukaribia?
Umpendaye na ambaye
wamjua jina?
Wanaokusifu,
Wanaokutii,
Wote wa’minifu moyoni,
Wasemao kweli.
3. Twakumiminia
yaliyo moyoni.
Unatuvuta, Watupenda,
Nawe watutunza.
Rafikizo wewe,
tunataka tuwe.
Wewe ni Rafiki mkuu,
hakuna mwingine.
(Ona pia Zab. 139:1; 1 Pet. 5:6, 7.)