WIMBO NA. 144
Kaza Macho Kwenye Zawadi!
Makala Iliyochapishwa
1. Watakapoona vipofu,
Nao viziwi wasikie,
Watoto watakapoimba,
Amani, shangwe ziwepo,
Wapendwa watafufuliwa,
Na kuishi pasipo dhambi.
(KORASI)
Utayaona mambo hayo,
Ukitazama zawadi.
2. Mbwa-mwitu, mwanakondoo
Watakula nyasi pamoja,
Naye mvulana mdogo,
Atawaongoza wote.
Hakutakuwa na machozi,
Mwisho wa maumivu, hofu.
(KORASI)
Utayaona mambo hayo,
Ukitazama zawadi.
(Ona pia Isa. 11:6-9; 35:5-7; Yoh. 11:24.)