Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 1/8 uku. 25
  • Kusitawi Licha ya Hali Ngumu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kusitawi Licha ya Hali Ngumu
  • Amkeni!—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Visiwa vya Canary—Tabia-Anga Tulivu, Mandhari Yenye Ushawishi
    Amkeni!—1994
  • Je, Matatizo Yako Ni Adhabu Kutoka kwa Mungu?
    Amkeni!—2009
  • Je, Matatizo Tunayopata Ni Adhabu Kutoka kwa Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Ulimwengu Uliojawa na Misiba
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2004
g04 1/8 uku. 25

Kusitawi Licha ya Hali Ngumu

Kama vile Biblia ilivyotabiri, tunaishi katika “nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.” (2 Timotheo 3:1) Matatizo ya familia, ya afya, na ya kifedha ni baadhi tu ya magumu ambayo huenda ukakabili. Nyakati nyingine, huenda ukahisi kwamba huwezi kuvumilia. Hata hivyo, unaweza kusitawi licha ya hali ngumu. Fikiria mfano ufuatao.

Ua aina ya Teide violet humea kwenye urefu wa meta 3,700 hivi katika kisiwa cha Tenerife karibu na pwani ya Afrika Kaskazini. Ua hilo limepewa jina la kilele cha mlima wa volkano ambao unapatikana katika sehemu kubwa ya kisiwa hicho. Kilele hicho kinaitwa Pico de Teide. Ni kana kwamba hakuna mimea yoyote kwenye sehemu za juu za mlima huo. Lakini katika majira ya kuchipua, theluji inayoyeyuka hutoa maji ya kutosha na kuwezesha maua hayo yachipuke na kupamba sehemu za juu za mlima kwa rangi ya zambarau. Naam, huenda ua hilo likaonekana kuwa dhaifu, lakini linaweza kustahimili hali ngumu za eneo hilo kame na hata kusitawi.

Kama ua la Teide violet, wewe pia unaweza kuvumilia licha ya hali ngumu. Biblia imewasaidia Mashahidi wa Yehova wengi kuvumilia nyakati ngumu sana. Kwa mfano, wale waliotiwa katika kambi za mateso za Ujerumani ya Nazi walivumilia. Mwandishi wa habari wa Sweden, Björn Hallström, anasema: “Walitendewa vibaya kuliko kikundi kingine chochote, lakini kwa sababu walimwamini Mungu, walivumilia kuliko wengine.”

Biblia inaweza kukusaidia kuvumilia hali yoyote ngumu. Ikiwa unataka kujifunza Biblia nyumbani kwako bila malipo, wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika eneo lenu au uwaandikie ukitumia anwani iliyo kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki