Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 9/09 uku. 20
  • Kuushika Kwelikweli Mkono wa Kuume wa Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuushika Kwelikweli Mkono wa Kuume wa Mungu
  • Amkeni!—2009
  • Habari Zinazolingana
  • Wamegundua Nini Huko Yezreeli?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Jiografia ya Biblia Je! Ni Sahihi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Rehema ya Mungu Kwa Wanadamu Katika Karne Yetu ya Ishirini
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • “Mimi, Yehova Mungu Wako, Ninaushika Mkono Wako wa Kuume”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2009
g 9/09 uku. 20

Kuushika Kwelikweli Mkono wa Kuume wa Mungu

◼ Jezreel anayeishi huko Mexico alizaliwa na ugonjwa wa ngozi usio wa kawaida unaoitwa congenital lamellar ichthyosis. Ugonjwa huo ulifanya ngozi yake ibambuke na kuwa ngumu. “Hilo hunifanya niwe na sura mbaya,” anaeleza Jezreel, “lakini ugonjwa huo hauwezi kuambukiza.”

Tangu Jezreel alipokuwa mtoto, alitibiwa katika hospitali mbalimbali. Alipokuwa na umri wa miaka miwili, aliwekwa katika chumba cha pekee ili asiambukizwe magonjwa mengine. Hata hivyo, hakuna kitu kilichoboresha ngozi yake. Alipewa matibabu ya kiakili ili kukabiliana na hisia zake za kukataliwa.

Mara nyingi, watu fulani humwepuka Jezreel kwa sababu wanadhani ugonjwa wake ni wa kuambukiza. Ilikuwa vigumu kwake kukabiliana na hali hiyo alipokuwa mtoto kwani alitaka kucheza na watoto wengine. Anasema, “Walinidhihaki na kuniita majina yenye kuumiza kama Maiti au Kiumbe kutoka sayari nyingine.”

Kwa upande mwingine, ugonjwa huo unaoonekana umempa Jezreel nafasi za kuwaeleza wengine kuhusu tumaini lake linalotegemea Biblia. Mara nyingi watu humwendea na kumwuliza ikiwa amechomeka. Anaposema hapana, wanamwuliza ni nini kilichofanya ngozi yake iwe hivyo. Anawaeleza kuhusu ugonjwa wake wa ngozi na kuwaambia kwamba kwa sasa hakuna tiba.

Kisha anaongeza, “Nina tumaini zuri zaidi ulimwenguni kwa kuwa Yehova Mungu anaahidi kwamba wale wanaotii sheria zake wataishi katika ulimwengu mpya usiokuwa na magonjwa na maumivu.” (Ufunuo 21:3, 4) Kuzungumzia hali yake kwa njia hiyo kumemsaidia Jezreel kuanzisha mafunzo ya Biblia, na amepata shangwe ya kuona baadhi yao wakianza kumwabudu Mungu.

Jezreel anasema, “Ninashukuru sana kwamba nilizaliwa katika familia ya Kikristo na kwamba nikiwa Shahidi wa Yehova, nina marafiki wa karibu. Hakuna yeyote aliyenikataa kwa sababu ya sura yangu. Nilibatizwa nikiwa na umri wa miaka 17 na kwa muda wa miaka 14 tangu nibatizwe, nimepata mapendeleo mengi ya kumtumikia Muumba wetu.”

Jezreel anakumbuka maneno yenye kutia moyo ya Yehova yanayopatikana katika Isaya 41:10, 13: “Usiogope, kwa maana mimi nipo pamoja nawe. . . . Nitakushika kwelikweli kwa mkono wangu wa kuume wa uadilifu. Kwa maana mimi, Yehova Mungu wako, ninaushika mkono wako wa kuume, Mwenye kukuambia, ‘Usiogope. Mimi mwenyewe nitakusaidia.’”

Kuushika kwelikweli mkono wa kuume wa Yehova kumemsaidia Jezreel kukabiliana na hisia za kujifikiria sana na kukabiliana na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wake. Pamoja na mamilioni ya wengine, anasubiri kutimizwa kwa ahadi nzuri ajabu za Mungu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki