Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/10 uku. 3
  • “Ninataka Talaka!”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Ninataka Talaka!”
  • Amkeni!—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Talaka Huwa na Majeruhi
    Amkeni!—1991
  • Ongezeko Kuu la Talaka
    Amkeni!—1992
  • Talaka Matokeo Yayo Mabaya
    Amkeni!—1992
  • Talaka Biblia Inasema Nini Hasa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2010
g 2/10 uku. 3

“Ninataka Talaka!”

Nyumba imechakaa kwa sababu ya kutotunzwa. Kwa miaka mingi imepigwa na dhoruba nyingi, na nyingine ziliidhoofisha. Sasa nyumba hiyo ni dhaifu, na inaonekana itaporomoka wakati wowote.

MFANO huo unaonyesha hali ya ndoa nyingi leo. Je, umewahi kuhisi kwamba ndoa yako inaelekea kuporomoka? Ikiwa ndivyo, uwe na hakika kwamba hakuna ndoa isiyokuwa na matatizo. Kwa kweli, Biblia inaeleza waziwazi kwamba wale wanaofunga ndoa yaelekea watapata “uchungu na huzuni.”—1 Wakorintho 7:28, The New English Bible.

Wakikazia ukweli wa maneno hayo, kikundi kimoja cha watafiti kinasema kwamba ndoa ndio “mradi hatari zaidi ambao watu wengi katika jamii yetu hujiingiza kwa ukawaida.” Kinaongezea hivi: “Uhusiano ambao huanza kwa shangwe na matumaini mengi unaweza kugeuka na kusababisha mfadhaiko na maumivu mengi maishani.”

Namna gani ndoa yako? Je, ina mojawapo ya matatizo haya?

  • Ugomvi wa kila mara

  • Maneno yenye kuumiza

  • Ukosefu wa uaminifu

  • Chuki

Ikiwa ndoa yako ni dhaifu na inaonekana kwamba itaporomoka wakati wowote, unapaswa kufanya nini? Je, talaka ndiyo suluhisho?

“TALAKA IMEKUWA JAMBO LA KAWAIDA”

Katika nchi fulani, idadi ya talaka imeongezeka sana. Fikiria nchi ya Marekani ambapo kwa miaka mingi, talaka haikuwa jambo la kawaida. Lakini katika kitabu chake The Divorce Culture, Barbara Dafoe Whitehead, anaandika kwamba baada ya mwaka wa 1960, “idadi ya talaka iliongezeka haraka sana.” Anasema: “Iliongezeka maradufu katika kipindi cha miaka 10 hivi na ikaendelea kuongezeka mpaka miaka ya mapema ya 1980 ilipofikia kilele chake kati ya jamii tajiri za nchi za Magharibi. Kwa sababu ya ongezeko hilo la haraka, katika kipindi cha miaka 30 tu, talaka imekuwa jambo la kawaida katika maisha ya Wamarekani.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki