Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 8/10 uku. 25
  • Bawa la Kereng’ende

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Bawa la Kereng’ende
  • Amkeni!—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Vito vya Kingo za Mto
    Amkeni!—1997
  • Bawa la Bundi
    Je, Ni Kazi ya Ubuni?
  • Fumbo la Kuruka kwa Wadudu Lafumbuliwa
    Amkeni!—1997
  • Sehemu ya Juu ya Bawa la Kipepeo
    Amkeni!—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2010
g 8/10 uku. 25

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Bawa la Kereng’ende

● Kereng’ende fulani wanaweza kusonga hewani bila kupiga mabawa kwa sekunde 30 bila kuteremka. Wanafanya hivyo jinsi gani? Kwa kutumia bawa ambalo ni tofauti sana na mabawa yaliyobuniwa na wataalamu wa ndege.

Fikiria hili: Bawa jembamba sana la kereng’ende lina mikunjo inayolizuia lisijipinde. Wanasayansi wameona kwamba mikunjo hiyo pia humsaidia kuinuka anaposonga bila kupiga mabawa. “Hiyo ni kwa sababu hewa hupita katika nafasi zilizo kati ya mikunjo na kutokeza maeneo yanayopitisha upepo na basi bawa linainuka,” linasema gazeti New Scientist.

Baada ya kuchunguza bawa la kereng’ende, injinia wa vyombo vya angani Abel Vargas na wenzake walikata kauli kwamba “mabawa ya viumbe ni muhimu sana kwa ubuni wa vyombo vidogo sana vinavyoruka.” Roboti hizo zenye ukubwa unaotoshana na kiganja, zilizo na kamera na vifaa vingine zinaweza kutumiwa kwa ajili ya mambo mengi, iwe ni kukusanya habari katika maeneo yaliyokumbwa na misiba au kuchunguza viwango vya uchafuzi.

Una maoni gani? Je, bawa jembamba sana, lenye mikunjo la kereng’ende lilijitokeza lenyewe? Au lilibuniwa?

[Picha katika ukurasa wa 25]

Roboti ndogo yenye umbo la kereng’ende ina uzito wa miligramu 120, upana wa sentimita sita, na mabawa membamba sana ya silikoni yanayopigapiga yanapotendeshwa na umeme

[Hisani]

© Philippe Psaila/Photo Researchers, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki