Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/12 kur. 28-29
  • Kumbuka Kusema Asante!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kumbuka Kusema Asante!
  • Amkeni!—2012
  • Habari Zinazolingana
  • Jitihada za Kutafuta Zawadi Bora
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Kwa Nini Uonyeshe Shukrani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • “Zawadi Iliyo Kubwa Zaidi”
    Amkeni!—1992
  • Je, Una Roho ya Kutoa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2012
g 7/12 kur. 28-29

Kumbuka Kusema Asante!

NI LINI mara ya mwisho ulipopokea kadi ya kukushukuru? Ni lini mara ya mwisho ulipotuma kadi kama hiyo?

Katika ulimwengu huu wa mawasiliano ya mtandao, taarifa za shukrani zilizoandikwa kwa mkono zinatoweka. Lakini, kusema “asante” kwa kutumia kalamu na karatasi ni njia ya pekee ya kuwajulisha watu kwamba unathamini fadhili wanazokuonyesha. Yafuatayo ni madokezo ya jinsi ya kufanya hivyo.

1. Andika kwa mkono wako mwenyewe badala ya kutumia taipureta au kompyuta.

2. Andika jina la mtu unayetaka kumshukuru.

3. Kama ulipokea zawadi, taja zawadi yenyewe na uonyeshe jinsi utakavyoitumia.

4. Mshukuru tena mwishoni mwa taarifa ya shukrani.

Kadi ya shukrani hugusa moyo wa aliyeandikiwa.

Hivyo basi, wakati ujao mtu fulani akikuonyesha ukarimu, kukufanyia tendo la fadhili, au kukupa zawadi, onyesha kwamba unathamini jitihada zake. Kumbuka kusema asante!

[Picha katika ukurasa wa 28, 29]

Shangazi Mpendwa Mary, (2)

Asante sana kwa ile saa iliyo na kengele! (3) Kwa sababu nina tatizo la kulala sana, tayari nimeanza kuitumia vizuri. Nilifurahi sana kukuona juma lililopita, na ninatumaini kwamba ulifika nyumbani salama. Tunatarajia kukuona tena hivi karibuni.

Kwa mara nyingine ninasema asante kwa zawadi hiyo, ulinifikiria sana! (4)

Mpwa wako,

John

[Picha]

(1)

[Sanduku katika ukurasa wa 29]

MADOKEZO

● Ikiwa ulipokea pesa kama zawadi usizitaje moja kwa moja. Kwa mfano, badala ya kutaja kiwango hususa cha pesa ulizopewa, unaweza kusema: “Asante kwa zawadi uliyonipa. Nitaitumia kwa ajili ya . . .”

● Andika tu habari inayohusiana na zawadi yenyewe na jinsi unavyoithamini. Usitumie fursa hiyo kufafanua jinsi ulivyofurahia likizo yako au mambo yaliyotendeka ulipoenda hospitali hivi karibuni.

● Usilalamike kuhusu tatizo lolote ulilopata kwa sababu ya zawadi uliyopewa. Kwa mfano, si jambo la fadhili kuandika, “Asante kwa shati ulilonipa—lakini ni kubwa mno!”

[Sanduku katika ukurasa wa 29]

Biblia inatutia moyo tuwe na roho ya kuonyesha shukrani. (Luka 17:11-19) Inatushauri ‘tusali bila kuacha’ kwa Mungu, ikiongezea kusema: “Kuhusiana na kila jambo toeni shukrani.”—1 Wathesalonike 5:17, 18.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki