Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g20 Na. 1 uku. 4
  • Ni Mambo Gani Husababisha Mkazo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Mambo Gani Husababisha Mkazo?
  • Amkeni!—2020
  • Habari Zinazolingana
  • Visababishi na Madhara ya Mfadhaiko
    Amkeni!—2005
  • Mkazo Mzuri, Mkazo Mbaya
    Amkeni!—1998
  • Jinsi ya Kudhibiti Mfadhaiko
    Amkeni!—2010
  • Ninaweza Kukabiliana Jinsi Gani na Mikazo Shuleni?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2020
g20 Na. 1 uku. 4

UNAWEZA KUKABILIANA NA MKAZO—JINSI GANI?

Ni Mambo Gani Husababisha Mkazo?

“Watu wengi wanasema kwamba wanazidi kupata mkazo,” kinaripoti kituo kimoja cha afya kinachojulikana sana. “Maisha ya leo yamejaa mabadiliko mengi na matukio yasiyotazamiwa.” Baadhi ya mabadiliko na matukio yasiyotazamiwa ambayo yanasababisha mkazo, yanatia ndani:

  • talaka

  • kifo cha mtu unayempenda

  • matatizo makubwa ya afya

  • aksidenti mbaya

  • uhalifu

  • shughuli zenye kuchosha za maisha

  • majanga—ya asili au yanayosababishwa na wanadamu

  • changamoto shuleni au kazini

  • kuhofia kupoteza kazi na kudumisha kipato

“KUPOTEZA KAZI,”

kunaweza kufadhaisha na kusababisha mtu aliyepoteza kazi apate matatizo ya afya, matatizo katika ndoa, mahangaiko, kushuka moyo na hata kujiua. Kupoteza kazi huathiri kila kitu maishani.”—American Psychological Association

MKAZO UTOTONI

Ni kawaida kwa watoto kuwa na mkazo. Baadhi ya watoto hunyanyaswa shuleni au kutelekezwa nyumbani. Wengine hutendewa vibaya kimwili, kihisia au kingono. Wengi wao huwa na wasiwasi kuhusu mitihani na alama wanazopata shuleni. Wengine hushuhudia familia zao zikigawanyika kwa sababu ya talaka. Watoto wenye mkazo huenda wakawa wanaota ndoto mbaya, wakawa na matatizo ya kujifunza, wakashuka moyo, au kuwa na tabia ya kujitenga na wengine. Baadhi yao hushindwa kudhibiti hisia zao. Mtoto aliye na mkazo anahitaji kusaidiwa haraka sana.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki