Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g20 Na. 1 kur. 14-15
  • Maisha Bila Mkazo Yanawezekana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maisha Bila Mkazo Yanawezekana
  • Amkeni!—2020
  • Habari Zinazolingana
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2020
  • Jinsi ya Kudhibiti Mfadhaiko
    Amkeni!—2010
  • Wakati Huo “Amani Itakuwa Nyingi”
    Amkeni!—2019
  • Mkazo Mzuri, Mkazo Mbaya
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2020
g20 Na. 1 kur. 14-15
Baba na mtoto wakicheza kwenye mawimbi ya bahari huku mama na binti wakifurahia kuwatazama wakiwa ufukweni.

UNAWEZA KUKABILIANA NA MKAZO—JINSI GANI?

Maisha Bila Mkazo Yanawezekana

Hekima inayopatikana katika Biblia inaweza kutusaidia kuepuka kuwa na mkazo kupita kiasi. Wanadamu hawawezi kuondoa kila kitu kinachosababisha mkazo. Lakini Muumba wetu ana uwezo wa kuondoa. Amemchagua Yesu Kristo ambaye anaweza kutusaidia tunapokabili mkazo. Hivi karibuni, atafanya mambo mazuri zaidi ulimwenguni pote kuliko yale aliyofanya alipokuwa hapa duniani. Kwa mfano:

YESU ATAPONYA WAGONJWA.

“Nao wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali . . . , naye akawaponya.” —MATHAYO 4:24.

YESU ATAANDAA CHAKULA NA MAKAZI KWA WATU WOTE.

“[Wale watakaotawaliwa na Kristo] watajenga nyumba na kuishi ndani yake, nao watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake. Hawatajenga na mtu mwingine akae ndani yake, wala hawatapanda na watu wengine wale.”—ISAYA 65:21, 22.

UTAWALA WA YESU UTALETA AMANI NA USALAMA ULIMWENGUNI POTE.

“Katika siku zake mwadilifu atasitawi, na amani itakuwa nyingi mpaka mwezi utakapokuwa haupo tena. Atakuwa na raia kutoka bahari mpaka bahari na kutoka Mto Efrati mpaka kwenye miisho ya dunia. . . . Maadui wake wataramba mavumbi.”—ZABURI 72:7-9.

YESU ATAKOMESHA UKOSEFU WA HAKI.

“Atamhurumia mtu wa hali ya chini na maskini, naye ataokoa uhai wa maskini. Atawaokoa kutoka katika ukandamizaji na ukatili.”—ZABURI 72:13, 14.

YESU ATAKOMESHA MATESO NA KIFO.

“Kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena.” —UFUNUO 21:4.

“NYAKATI ZA HATARI ZILIZO NGUMU KUSHUGHULIKA NAZO”

“Leo, ulimwengu umejaa mikazo, hofu, huzuni, na maumivu mengi kuliko wakati mwingine wowote.”—Mohamed S Younis, mhariri wa shirika la Gallup.

Kwa nini watu wengi leo wana mkazo? Biblia inatupatia jibu lenye kuridhisha. Andiko la 2 Timotheo 3:1 linasema: “Katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.” Biblia inataja sababu kwa kuonyesha jinsi ambavyo watu wangejiendesha vibaya. Tabia zao zinatia ndani pupa, kiburi, unafiki wa dini, jeuri, kutokuwa na upendo katika familia, na kutojizuia. (2 Timotheo 3:2-5) Siku za mwisho zitaisha wakati Yesu Kristo atakapotawala dunia akiwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu, serikali itakayotawala kutoka mbinguni.—Danieli 2:44.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki