Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w10 3/1 kur. 24-25
  • Somo Kuhusu Rehema ya Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Somo Kuhusu Rehema ya Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Mtu Mwenye Unyenyekevu na Ujasiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Uharibifu wa Sodoma na Gomora
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Anawaponya Watu Kimuujiza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Yesu Awashangaza Wasikilizaji Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
w10 3/1 kur. 24-25

Kwa Ajili ya Vijana Wetu

Somo Kuhusu Rehema ya Mungu

YONA—SEHEMU YA 2

Maagizo: Fanya zoezi hili katika mazingira matulivu. Unaposoma maandiko, jiwazie ukiwa katika matukio yanayozungumziwa. Wazia kikao. Sikia sauti. Hisi kama wahusika wakuu wanavyohisi. Wazia kwamba masimulizi haya ni halisi kabisa.

1 CHUNGUZA TUKIO HILI.—SOMA YONA 3:1–4:11.

Unafikiria Yona alihisi jinsi gani alipokuwa akiingia katika jiji la Ninawi?

․․․․․

Unafikiria sauti ya Yona ilionyesha hisia gani alipokuwa akitangaza hukumu ya Yehova?

․․․․․

Inaonekana Yona alikuwa akisumbuliwa na nini alipokuwa ameketi nje ya jiji? (Soma Yona 4:5-8.)

․․․․․

2 CHIMBA ZAIDI.

Kwa nini huenda Yona alitaka Yehova aharibu Ninawi kama alivyokuwa ametabiri?

․․․․․

Ukitumia vifaa vya utafiti unavyoweza kupata, chunguza kuhusu (1) mmea wa mtango na jinsi ulivyoonekana, na (2) kwa nini mfalme wa Ninawi alijifunika nguo za magunia na kuketi katika majivu.

․․․․․

Ingawa mwanzoni Yona alikataa kutoa unabii huko Ninawi, kwa nini anaweza kuitwa nabii mwaminifu na mwenye ujasiri? (Mathayo 21:28-31)

․․․․․

3 TUMIA MAMBO ULIYOJIFUNZA. ANDIKA MAMBO ULIYOJIFUNZA KUHUSU . . .

Uwezekano wa wanadamu kuacha maisha mapotovu.

․․․․․

Rehema ya Yehova.

․․․․․

Kwa nini tunahitaji kuonyesha rehema.

․․․․․

4 NI MAMBO GANI KATIKA SIMULIZI HILI AMBAYO YAMEKUGUSA MOYO SANA, NA KWA NINI?

․․․․․

Ili ufanye utafiti zaidi, ona gazeti la Mnara wa Mlinzi la Aprili 1, 2009 (1/4/2009), ukurasa wa 14-18.

SOMA HABARI ZAIDI ZA BIBLIA, KWENYE INTANETI www.watchtower.org

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki