Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w15 10/1 uku. 16
  • Majibu ya Maswali ya Biblia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Majibu ya Maswali ya Biblia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Wafungwa wa Umaskini
    Amkeni!—1998
  • Jitihada za Kumaliza Umaskini
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Mwisho wa Umaskini Wakaribia
    Amkeni!—1998
  • Habari Njema Kwa Maskini
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
w15 10/1 uku. 16

MAJIBU YA MASWALI YA BIBLIA

Je, umaskini utaisha?

Mwanamke ameshika bakuli isiyo na kitu na amemkumbatia binti yake

Mungu ataondoa jinsi gani umaskini ulimwenguni?—Mathayo 6:9, 10.

Ufukara unaosababisha utapiamlo na magonjwa huua mamilioni ya watu kila mwaka. Ingawa nchi nyingi zimeendelea kiuchumi, idadi kubwa ya watu ni maskini sana. Biblia inaonyesha kwamba umaskini umekuwapo kwa muda mrefu.—Soma Yohana 12:8.

Ili kuondoa umaskini ni lazima kuwe na serikali yenye uwezo wa kugawa kwa haki rasilimali za dunia. Serikali hiyo itahitaji kukomesha vita ambavyo ni chanzo kikubwa cha umaskini. Mungu ameahidi kuleta serikali hiyo.—Soma Danieli 2:44.

Ni nani atakayeondoa umaskini?

Mungu amemchagua Mwana wake, Yesu, atawale wanadamu. (Zaburi 2:4-8) Yesu atawakomboa maskini na kukomesha ukandamizaji na jeuri.—Soma Zaburi 72:8, 12-14.

Akiwa “Mkuu wa Amani” aliyetabiriwa, Yesu ataleta amani na usalama duniani. Watu wote wataishi katika nyumba zao, watafurahia kufanya kazi, na kutakuwa na chakula kingi.—Soma Isaya 9:6, 7; 65:21-23.

Kwa habari zaidi, soma sura ya 8 ya kitabu hiki, Biblilia Inafundisha Nini Hasa?, kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova

Pia kinapatikana kwenye www.jw.org/sw

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki