Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp16 Na. 5 uku. 3
  • Tunahitaji Faraja

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tunahitaji Faraja
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Habari Zinazolingana
  • Faraja Wakati wa Matatizo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Wafariji Wale Wanaohuzunika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Faraja kwa Watu Waliotendewa Vibaya Kingono
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Liwazo Kutoka kwa “Mungu wa Faraja Yote”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
wp16 Na. 5 uku. 3

HABARI KUU | UNAWEZA KUPATA WAPI FARAJA?

Tunahitaji Faraja

Mama akimfariji mtoto wake

Je, unakumbuka ulipoanguka ukiwa mtoto? Huenda uliumia mkono au mguu. Je, unakumbuka jinsi ambavyo mama alikufariji? Labda, alisafisha kidonda na kisha kukifunga kwa bendeji. Ingawa ulilia, ulihisi nafuu alipokukumbatia na kukufariji. Wakati huo, ilikuwa rahisi kupata mtu wa kukufariji.

Hata hivyo, kadiri tunavyoendelea kukua tunakabili changamoto zaidi maishani. Matatizo yanakuwa mengi, na inakuwa vigumu kupata faraja. Inasikitisha kwamba matatizo ambayo watu wazima hukabili hayawezi kwisha kwa kufungwa bendeji au kukumbatiwa. Fikiria mifano kadhaa.

  • Je, umewahi kupata mkazo kwa sababu ya kupoteza kazi? Julian anasema kwamba alipata mkazo baada ya kufutwa kazi. Aliwaza hivi, ‘Nitawezaje kuitunza familia yangu? Kwa nini kampuni imeniachisha kazi ingawa nimekuwa mfanyakazi mzuri kwa miaka mingi?’

  • Huenda unakabili changamoto kwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa yako. Raquel anasema hivi: “Nilihuzunika sana, mume wangu aliponiacha miezi 18 iliyopita. Nilivunjika moyo sana. Niliumia kimwili na kihisia pia. Hilo liliniogopesha sana.”

  • Huenda una ugonjwa wa kudumu. Labda nyakati fulani unahisi kama Ayubu ambaye alisema hivi kwa uchungu: “Nimekataa huo; sitaishi mpaka wakati usio na kipimo.” (Ayubu 7:16) Huenda ukakubaliana na maoni ya Luis, mwanamume mwenye umri wa miaka 80 hivi aliyesema, “Nyakati nyingine mimi huhisi kana kwamba ninangojea kufa tu.”

  • Au huenda unatamani kufarijiwa kwa sababu umefiwa na mtu unayempenda. Robert anasema: “Mwanzoni sikuamini nilipopata habari kwamba mwanangu amekufa katika aksidenti ya ndege. Kisha niliumia sana, maumivu ambayo Biblia huyafananisha na upanga mrefu unaochoma nafsi.”—Luka 2:35.

Licha ya hali hizo ngumu, Robert, Luis, Raquel, na Julian wamepata faraja. Wamepata Yule anayeweza kuwafariji, yaani, Mungu Mwenye enzi kuu ambaye ni chanzo cha faraja. Mungu huandaa faraja jinsi gani? Je, anaweza kukufariji?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki