Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp17 Na. 6 uku. 3
  • “Ilikuwa Zawadi Bora Niliyowahi Kupokea”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Ilikuwa Zawadi Bora Niliyowahi Kupokea”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Habari Zinazolingana
  • Jitihada za Kutafuta Zawadi Bora
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Je, Una Roho ya Kutoa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Zawadi Bora Zaidi ya Mungu​—Kwa Nini Ni Yenye Thamani Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • “Zawadi Iliyo Kubwa Zaidi”
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
wp17 Na. 6 uku. 3
Binti akiwa na mnyama anayempenda, mwanamke akiwa na kompyuta, mwanamume akiwa na kadi aliyotengenezewa na mke wake

HABARI KUU | NI ZAWADI GANI BORA KULIKO ZOTE?

“Ilikuwa Zawadi Bora Niliyowahi Kupokea”

Binti mwenye umri wa miaka 13 alihisi hivyo baada ya kupokea zawadi ya mnyama anayempenda. Mwanamke fulani ambaye ni mfanyabiashara mwenye mafanikio alisema kwamba zawadi ya kompyuta aliyopewa na baba yake alipokuwa shule ya sekondari, ilibadili maisha yake. Mwanamume aliyeoa hivi karibuni anahisi kwamba kadi aliyotengenezewa na mke wake walipotimiza mwaka mmoja wa ndoa, ilikuwa zawadi bora aliyowahi kupokea.

Kila mwaka, watu hutumia muda na jitihada nyingi wakitafuta zawadi “bora” ya kumpatia rafiki au mtu wa ukoo katika matukio ya pekee. Na wengi wao wangependa kusikia maneno kama yale yaliyo kwenye kichwa cha makala hii. Namna gani wewe? Je, ungependa kupokea au kutoa zawadi ambayo itathaminiwa?

Tarajio hilo linapendeza sana, kwa sababu ya jinsi linavyofanya mtoaji na mpokeaji wahisi. Haishangazi kwamba Biblia inasema: “Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.” (Matendo 20:35) Bila shaka, tutapata furaha zaidi ikiwa zawadi tunayotoa inathaminiwa na yule tunayempatia.

Hivyo basi, unapotoa zawadi, unaweza kufanya nini ili wewe na yule anayeipokea mpate furaha zaidi? Na ingawa si rahisi kutoa zawadi “bora,” unaweza kufanya nini ili zawadi yako ithaminiwe?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki