Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/10 uku. 3
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2010
Huduma Yetu ya Ufalme—2010
km 4/10 uku. 3

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Aprili 26, 2010. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 20 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Machi 1 hadi Aprili 26, 2010.

1. Naomi alimaanisha nini aliposema, “Yehova ndiye amenifedhehesha na Mweza-Yote ndiye amenisababishia msiba?” (Rut. 1:21) [w05 3/1 uku. 27 fu. 2, 4]

2. Ni sifa gani zilizomfanya Ruthu awe “mwanamke bora sana”? (Rut. 3:11) [w05 3/1 uku. 28 fu. 6]

3. Maneno ya Elkana, “Je, mimi si bora kwako kuliko wana kumi” yalimwimarisha mke wake jinsi gani? (1 Sam. 1:8) [w90 3/15 uku. 27 fu. 5-6]

4. Kwa nini haikufaa Waisraeli waombe kupewa mfalme? (1 Sam. 8:5) [w05 9/15 uku. 20 fu. 17; it-2-E uku. 163 fu. 1]

5. Samweli ‘aliyekuwa amezeeka na mwenye mvi,’ alikuwa mfano mzuri kwa njia gani kuhusiana na kusali kwa ajili ya wengine, na jambo hili linakazia nini? (1 Sam. 12:2, 23) [w07 6/1 uku. 29 fu. 13-15]

6. Kwa nini Sauli aliwaonyesha Wakeni fadhili kwa njia ya pekee? (1 Sam. 15:6) [w05 3/15 uku. 22 fu. 10]

7. Kwa nini Sauli alimwuliza Daudi, “Wewe ni mwana wa nani?” (1 Sam. 17:58) [w07 8/1 uku. 31 fu. 3, 5]

8. Tunajifunza nini kutokana na jinsi Daudi alivyoshughulikia tatizo kubwa huko Gathi? (1 Sam. 21:12, 13) [w05 3/15 uku. 24 fu. 4]

9. Yonathani alionyeshaje upendo na unyenyekevu alipohitaji kumwunga mkono na kumtia moyo rafiki yake Daudi? (1 Sam. 23:17) [lv uku. 28 fu. 10, maelezo ya chini.]

10. Tunajifunza nini kutokana na simulizi kumhusu Sauli alipomwendea mchawi wa En-dori? (1 Sam. 28:8-19) [w05 3/15 uku. 24 fu. 7; sp uku. 15 fu. 1, 2]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki