Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Februari 28, 2011. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 20 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Januari 3 hadi Februari 28, 2011.
1. Hezekia alianzisha kazi gani mwanzoni mwa utawala wake, na tunaweza kumwigaje leo? (2 Nya. 29:16-18) [w09 6/15 uku. 9 fu. 13]
2. Andiko la 2 Mambo ya Nyakati 36:21 linaonyeshaje utimizo wa unabii unaopatikana katika Yeremia 25:8-11? [w06 11/15 uku. 32 fu. 1-4]
3. Kitabu cha Ezra 3:1-6 kinaungaje mkono uthibitisho wa Kimaandiko kwamba kipindi cha miaka 70 cha ukiwa wa Yerusalemu kiliisha kwa wakati? [w06 1/15 uku. 19 fu. 3]
4. Kwa nini Ezra alishtuka alipopata habari kwamba Waisraeli walikuwa wakifunga ndoa pamoja na watu wa nchi? (Ezra 9:1-3) [w06 1/15 uku. 20 fu. 1]
5. Ni nani waliokuwa watu “mashuhuri,” na tunapaswa kuepuka mtazamo gani waliokua nao? (Neh. 3:5) [w06 2/1 uku. 10 fu. 2; w86 2/15 uku. 21]
6. Gavana Nehemia ni mfano mzuri kwa waangalizi Wakristo jinsi gani? (Neh. 5:14-19) [si uku. 90 fu. 16]
7. Kama Waisraeli wa siku za Nehemia, tunaweza kuepukaje kuipuuza “nyumba ya Mungu wetu”? (Neh. 10:32-39) [w98 10/15 uku. 21-22 fu. 12]
8. Kutafakari kuhusu mwendo wa Nehemia kunaweza kutufanya tujiulize maswali gani? (Neh. 13:31) [w96 9/15 uku. 16 fu. 3]
9. Je, Esta alifanya uasherati na Mfalme Ahasuero? (Esta 2:14-17) [w91 1/1 uku. 31 fu. 6]
10. Kwa nini Mordekai alikataa kumwinamia Hamani? (Esta 3:2, 4) [it-2-E uku. 431 fu. 7; w06 3/1 uku. 9 fu. 4]