HAZINA ZA NENO LA MUNGU
“Nyumba Yote ya Ahabu Itaangamia”—2Fa 9:8
UFALME WA YUDA
Yehoshafati anatawala
m. 911 K.W.K.: Yehoramu (mwana wa Yehoshafati; mume wa Athalia, binti ya Ahabu na Yezebeli) anaanza kutawala akiwa mfalme peke yake
m. 906 K.W.K.: Ahazia (mjukuu wa Ahabu na Yezebeli) anakuwa mfalme
m. 905 K.W.K.: Athalia anawaua wazao wote wa kifalme na kujinyakulia ufalme. Yehoashi, mjukuu wake ndiye tu anayeokolewa na kufichwa na Kuhani Mkuu Yehoyada.—2Fa 11:1-3
898 K.W.K.: Yehoashi anakuwa mfalme. Malkia Athalia anauawa na Kuhani Mkuu Yehoyada.—2Fa 11:4-16
UFALME WA ISRAELI
m. 920 K.W.K.: Ahazia (mwana wa Ahabu na Yezebeli) anakuwa mfalme
m. 917 K.W.K.: Yehoramu (mwana wa Ahabu na Yezebeli) anakuwa mfalme
m. 905 K.W.K.: Yehu anamuua Mfalme Yehoramu wa Israeli na ndugu zake, mama ya Yehoramu (Yezebeli), na Mfalme Ahazia wa Yuda na ndugu zake.—2Fa 9:14–10:17
m. 904 K.W.K.: Yehu anaanza kutawala akiwa mfalme