Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Wafalme 11
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

2 Wafalme—Yaliyomo

      • Athalia aunyakua ufalme (1-3)

      • Yehoashi awekwa kisiri kuwa mfalme (4-12)

      • Athalia auawa (13-16)

      • Mabadiliko yaliyofanywa na Yehoyada (17-21)

2 Wafalme 11:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yote ya ufalme.”

Marejeo

  • +2Fa 8:26; 11:20; 2Nya 21:5, 6; 24:7
  • +2Fa 9:27
  • +2Nya 21:4; 22:10-12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Ufahamu,

2 Wafalme 11:2

Marejeo

  • +2Fa 12:1

2 Wafalme 11:4

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “wakimbiaji.”

  • *

    Au “agano.”

Marejeo

  • +1Fa 14:27
  • +2Nya 23:1-3

2 Wafalme 11:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “jumba la.”

Marejeo

  • +1Fa 7:1; 2Nya 23:4-7

2 Wafalme 11:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “anapotoka nje na anapoingia ndani.”

2 Wafalme 11:9

Marejeo

  • +2Fa 11:4
  • +2Nya 23:8-11

2 Wafalme 11:11

Marejeo

  • +1Fa 14:27
  • +1Fa 8:22; 2Nya 4:1

2 Wafalme 11:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Labda ni kitabu cha kukunjwa kilichokuwa na Sheria ya Mungu.

Marejeo

  • +2Fa 11:2
  • +Kut 25:21; 31:18
  • +1Fa 1:39, 40

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    2/1/1991, uku. 31

2 Wafalme 11:13

Marejeo

  • +2Nya 23:12-15

2 Wafalme 11:14

Marejeo

  • +2Fa 23:3
  • +2Nya 5:12

2 Wafalme 11:15

Marejeo

  • +2Fa 11:4; 2Nya 23:9

2 Wafalme 11:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “jumba la.”

Marejeo

  • +1Fa 7:1

2 Wafalme 11:17

Marejeo

  • +1Sa 10:25; 2Sa 5:3
  • +2Nya 23:16, 17

2 Wafalme 11:18

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “hekalu la.”

Marejeo

  • +Kum 12:3
  • +Kum 7:25
  • +Kum 13:5
  • +2Nya 23:18-21

2 Wafalme 11:19

Marejeo

  • +2Fa 11:4, 15
  • +1Fa 14:27
  • +2Sa 7:8, 16

2 Wafalme 11:21

Marejeo

  • +2Fa 11:2
  • +2Nya 24:1

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

2 Fal. 11:12Fa 8:26; 11:20; 2Nya 21:5, 6; 24:7
2 Fal. 11:12Fa 9:27
2 Fal. 11:12Nya 21:4; 22:10-12
2 Fal. 11:22Fa 12:1
2 Fal. 11:41Fa 14:27
2 Fal. 11:42Nya 23:1-3
2 Fal. 11:51Fa 7:1; 2Nya 23:4-7
2 Fal. 11:92Fa 11:4
2 Fal. 11:92Nya 23:8-11
2 Fal. 11:111Fa 14:27
2 Fal. 11:111Fa 8:22; 2Nya 4:1
2 Fal. 11:122Fa 11:2
2 Fal. 11:12Kut 25:21; 31:18
2 Fal. 11:121Fa 1:39, 40
2 Fal. 11:132Nya 23:12-15
2 Fal. 11:142Fa 23:3
2 Fal. 11:142Nya 5:12
2 Fal. 11:152Fa 11:4; 2Nya 23:9
2 Fal. 11:161Fa 7:1
2 Fal. 11:171Sa 10:25; 2Sa 5:3
2 Fal. 11:172Nya 23:16, 17
2 Fal. 11:18Kum 12:3
2 Fal. 11:18Kum 7:25
2 Fal. 11:18Kum 13:5
2 Fal. 11:182Nya 23:18-21
2 Fal. 11:192Fa 11:4, 15
2 Fal. 11:191Fa 14:27
2 Fal. 11:192Sa 7:8, 16
2 Fal. 11:212Fa 11:2
2 Fal. 11:212Nya 24:1
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
2 Wafalme 11:1-21

Kitabu cha Pili cha Wafalme

11 Basi Athalia+ mama ya Ahazia alipoona kwamba mwanawe amekufa,+ alitoka na kuangamiza uzao wote wa kifalme.*+ 2 Hata hivyo, Yehosheba binti ya Mfalme Yehoramu, dada ya Ahazia, akamchukua Yehoashi+ mwana wa Ahazia, akamwiba kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliopaswa kuuawa na kumweka yeye pamoja na mlezi wake katika chumba cha ndani cha kulala. Wakafanikiwa kumficha ili Athalia asimwone, kwa hiyo hakuuawa. 3 Akakaa pamoja naye kwa miaka sita akiwa amefichwa katika nyumba ya Yehova, Athalia alipokuwa akitawala nchi.

4 Katika mwaka wa saba, Yehoyada aliagiza wakuu wa mamia wa walinzi walioitwa Wakari na wa walinzi* wa jumba la mfalme+ waitwe, wakaja kwake katika nyumba ya Yehova. Akafanya mapatano* pamoja nao na kuwaapisha kuhusu mapatano hayo katika nyumba ya Yehova, kisha akawaonyesha mwana wa mfalme.+ 5 Akawapa agizo hili: “Hivi ndivyo mtakavyofanya: Theluthi moja watashika zamu siku ya Sabato, na kuweka ulinzi mkali katika nyumba ya* mfalme,+ 6 theluthi nyingine watakuwa katika Lango la Msingi, na theluthi nyingine watakuwa katika lango lililo nyuma ya walinzi wa jumba la mfalme. Mtalinda nyumba hiyo kwa zamu. 7 Vikundi vyenu viwili ambavyo havipaswi kuwa na zamu siku ya Sabato vinapaswa kuweka ulinzi mkali katika nyumba ya Yehova ili kumlinda mfalme. 8 Mnapaswa kumzunguka mfalme pande zote, kila mmoja akiwa na silaha zake mikononi mwake. Yeyote atakayekaribia kikosi hicho atauawa. Mfuateni mfalme popote aendapo.”*

9 Wakuu wa mamia+ wakafanya sawasawa na alivyoamuru kuhani Yehoyada. Basi kila mmoja wao akachukua wanaume wake waliokuwa na zamu siku ya Sabato, pamoja na wale ambao hawakuwa na zamu siku ya Sabato, wakaja kwa kuhani Yehoyada.+ 10 Kisha kuhani akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao za mviringo zilizokuwa za Mfalme Daudi, ambazo zilikuwa katika nyumba ya Yehova. 11 Na walinzi wa jumba la mfalme+ wakasimama mahali pao, kila mmoja akiwa na silaha zake mikononi, kuanzia upande wa kulia wa nyumba mpaka upande wa kushoto wa nyumba, kando ya madhabahu,+ na kando ya nyumba hiyo, kumzunguka mfalme pande zote. 12 Kisha Yehoyada akamtoa nje mwana wa mfalme+ na kumvika taji na Ushahidi,*+ wakamweka kuwa mfalme na kumtia mafuta. Wakaanza kupiga makofi na kusema: “Mfalme na aishi muda mrefu!”+

13 Athalia aliposikia sauti ya watu wakikimbia, mara moja akaja na kujiunga na watu katika nyumba ya Yehova.+ 14 Kisha akamwona mfalme akiwa amesimama hapo kando ya nguzo kama ilivyokuwa desturi.+ Wakuu na wapiga tarumbeta+ walikuwa pamoja na mfalme, na watu wote nchini walikuwa wakishangilia na kupiga tarumbeta. Ndipo Athalia akayararua mavazi yake na kupaza sauti: “Ni njama! Ni njama!” 15 Lakini kuhani Yehoyada akawaamuru hivi wakuu wa mamia,+ wale waliowekwa kulisimamia jeshi: “Mwondoeni miongoni mwa vikosi, na yeyote akimfuata, muueni kwa upanga!” Kwa maana kuhani alikuwa amesema: “Msimuue ndani ya nyumba ya Yehova.” 16 Basi wakamkamata, na alipofika mahali ambapo farasi huingia katika nyumba ya* mfalme,+ akauawa hapo.

17 Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Yehova na mfalme na watu,+ kwamba wataendelea kuwa watu wa Yehova, pia akafanya agano kati ya mfalme na watu.+ 18 Baada ya hayo, watu wote nchini wakaenda kwenye nyumba ya* Baali na kubomoa madhabahu zake,+ nao wakazivunja kabisa sanamu zake,+ na kumuua Matani kuhani wa Baali+ mbele ya madhabahu.

Halafu kuhani akawaweka waangalizi wa nyumba ya Yehova.+ 19 Tena, akawachukua wakuu wa mamia,+ walinzi walioitwa Wakari, walinzi wa jumba la mfalme,+ na watu wote nchini ili wamsindikize mfalme kushuka kutoka katika nyumba ya Yehova, wakaja katika jumba la mfalme kupitia lango la walinzi wa jumba la mfalme. Kisha mfalme akaketi kwenye kiti cha wafalme.+ 20 Basi watu wote nchini wakashangilia na jiji likatulia, kwa maana walikuwa wamemuua Athalia kwa upanga katika jumba la mfalme.

21 Yehoashi+ alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki