Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwbq makala 41
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Kutiwa Damu Mishipani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Kutiwa Damu Mishipani?
  • Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jibu la Biblia
  • Heshima ya Kimungu kwa Uhai na Damu
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Kuokoa Uhai kwa Damu—Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Azimio Letu Imara Juu ya Uhai na Damu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Damu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
Pata Habari Zaidi
Maswali ya Biblia Yajibiwa
ijwbq makala 41

Biblia Inasema Nini Kuhusu Kutiwa Damu Mishipani?

Jibu la Biblia

Biblia inatuamuru tusile damu. Kwa hiyo, hatupaswi kukubali damu nzima au sehemu zake za msingi kwa njia yoyote ile, iwe tunaila kama chakula au tunatiwa mishipani. Fikiria maandiko yafuatayo:

  • Mwanzo 9:4. Baada ya Gharika, Mungu alimruhusu Noa na familia yake kula nyama lakini akawaamuru wasile damu. Mungu alimwambia hivi Noa: “Isipokuwa tu nyama pamoja na nafsi yake—damu yake—msile.” Amri hiyo inawahusu pia wanadamu wote kuanzia wakati huo na kuendelea kwa kuwa wote ni wazao wa Noa.

  • Mambo ya Walawi 17:14. “Hamtakula damu ya mwili wa namna yoyote, kwa sababu nafsi ya kila mwili wa namna yoyote iko katika damu yake. Mtu yeyote atakayeila atakatiliwa mbali.” Mungu aliona nafsi, au uhai, umo katika damu na ni mali yake. Ijapokuwa taifa la Israeli ndilo lililopewa sheria hiyo, inaonyesha kwamba Mungu alichukua kwa uzito sana sheria ya kutokula damu.

  • Matendo 15:20. ‘Jiepusheni na damu.’ Mungu aliwapa Wakristo amri hiyohiyo aliyompa Noa. Historia inaonyesha kwamba Wakristo wa mapema walikataa kula damu nzima, hata ikiwa ni kwa ajili ya matibabu.

Kwa nini Mungu anatuamuru tujiepushe na damu?

Kuna sababu nzuri za kimatibabu za kuepuka kutiwa damu mishipani. Hata hivyo, sababu muhimu zaidi ya Mungu kutuamuru tujiepushe na damu ni kwamba inawakilisha kitu kitakatifu machoni pake.—Mambo ya Walawi 17:11; Wakolosai 1:20.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki