Kujikumbusha Kwa Kuandika Kwa Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Kujikumbusha vitabu vikiwa vyenye kufungwa kwa mambo yaliyozungumzwa kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma toka Januari 6 mpaka lile la Aprili 21, 1997. Jibu kwa kutumia karatasi tofauti kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Agizo: Wakati wa kujikumbusha, tumia tu Biblia. Mitajo inayotolewa kisha kila ulizo inatolewa ili kurahisisha utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu hazionyeshwi kila mara kuhusu mitajo ya Mnara wa Mlinzi.]
Jibu Kweli au Si Kweli kisha sentensi zifuatazo:
1. Miaka kabla ya kuundwa kwa Shule ya Biblia ya Gileadi, habari njema ilipelekwa ugenini na Mashahidi walioujua ukweli katika nchi nyingine na waliorudi katika nchi yao ya asili ili kuhubiri huko. [jv uku. 428 fu. 2]
2. Gideoni aliweza kushinda Wamidiani kwa msaada wa nguvu za kijeshi. [ad uku. 578 maf. 3-4]
3. Katika utimizo wa Zekaria 9:2-4, Tiro uliharibiwa kabisa kabisa na Nebukadreza. [siSW uku. 169 fu. 4]
4. Je! Hawa alikuwa na sababu ya kusema kwamba alipata mtoto mwanamume (Kaini) “kwa msaada wa Yehova”? (Mwa. 4:1) [ad uku. 505 fu. 7]
5. Charles Russel alijulikana kuwa msemaji mashuhuri, lakini ni kupendezwa kwa kweli kweli ambako alikuwa nako kwa watu ndiko kulimfanya kuwa mwevanjelisti mwenye matokeo. [jv uku. 404 fu. 2]
6. Watu weusi hawatokani na Kanaani, mwana wa Shemu, ambaye Noa alilaani. [ad uku. 257 fu. 6]
7. Kati ya “mbuzi” ambao wanazungumziwa katika Mathayo 25:31-46, ambao watakatiliwa mbali milele, kutakuwa ndani washiriki wenye kutenda wa Babuloni Mkuu na viongozi wao wa kidini. [Usomaji wa Biblia; ona wSW95 10/15 uku. 26 maf. 13-15.]
8. Kwa sababu ya mateso makali yaliyotokea katika Ulaya, hesabu ya wahubiri ilipunguka sana sana katika nchi hizo wakati wa Vita ya Pili ya Ulimwengu. [jv uku. 454 fu. 2]
9. Msamaha tunaotolea wengine unawezesha msamaha wa dhambi zetu kwa Mungu. [Usomaji wa Biblia; ona wSW94 9/15 uku. 7.]
10. Gabrieli ni mmoja wa malaika wawili tu waaminifu ambao Biblia inamwita kwa jina lake. [ad uku. 563 fu. 11]
Jibu maulizo yafuatayo:
11. Katika 1938, ni ufundi gani wenye kusisimua uliotumiwa katika Uingereza, Landani, kwa kutangaza hotuba ya kusanyiko yenye kichwa: “Kukabiliana na Uhakika”? [jv uku. 447 fu. 2]
12. Ni vyeo gani viwili vya Yesu Kristo ambavyo vilielezwa katika Zekaria 6:12, 13? [siSW uku. 172 fu. 25]
13. Mpango wa kuomba makutaniko kutoa michango kwenye Fedha za Sosaiti kwa ajili ya Majumba ya Ufalme unaonyesha matumizi ya kanuni gani? [jv uku. 344 maf. 3-4]
14. Namna gani dhabihu ya Yesu tayari inatokeza faida kwa wanadamu? [klSW kur. 68-9 maf. 17-19]
15. Kwa nini hatungepaswa kusita kufasiria kwa wasikilizaji wetu kwamba kazi yetu inategemezwa na michango ya kujipendea? [jv uku. 349 fu. 4]
16. Katika utimizo wa Malaki 4:5, ni katika maana gani “nabii Eliya” alitokea katika karne ya kwanza? [siSW uku. 174 fu. 15]
17. Jinsi gani dhambi ilienea kwa wanadamu wote? [klSW uku. 58 fu. 13]
18. Ni katika maandiko gani ya kitabu cha Mathayo tunapata mashauri yenye akili ambayo Yesu alitoa juu ya namna ya kutatua mambo magumu? [Usomaji wa Biblia; ona wSW95 7/15 uku. 22.]
19. “Dinari” ambayo Yesu alisema katika mfano wake unaoripotiwa katika Mathayo 20:1-16 humaanisha nini? [Usomaji wa Biblia; ona gtSW 97 fu. 6.]
20. Taja mambo mawili yaliyoonyeshwa wazi na kuruhusu kwa Mungu ubaya. [klSW kur. 77-8 maf. 18-20]
Jaza nafasi zilizo wazi katika sentensi zifuatazo:
21. Gospeli (injili) tatu za kwanza huitwa “sainoptiki”, jambo linaloomaanisha _________________________ . [siSW uku. 175 fu. 3]
22. Kwa pupa, _________________________ mtumishi wa Elisha, alitafuta kupata faida ya kimwili wakati bwana wake alipoponyesha ukoma wa _________________________ . [ad uku. 623 fu. 5]
23. Kwa kuwa alikataa kujali onyo lililotolewa na wakuu wa nguvu za kijeshi, _________________________ aliuwawa na Yishmaeli na watu wake. [ad uku. 622 fu. 8]
24. Yehova alitumia manabii _________________________ na _________________________ ili kuchochea shauku ya watu wake kwa ajili ya kujenga upya hekalu. [ad uku. 39 maf. 6-7]
25. “Roho” inayowatoka wanadamu wakati wa kifo ni _________________________ . inayotoka kwa Mungu. (Zab. 146:4). [klSW uku. 81 maf. 5-6]
Onyesha majibu ya kweli katika habari zifuatazo:
26. Kuna uhakikisho mbalimbali unaoonyesha kwamba Mathayo aliandika gospeli yake katika (Kiebrania; Kiaramu; Kigiriki) na aliitafsiri baadaye katika (Kiebrania, Kiaramu; Kigiriki). [siSW uku. 176 fu. 6]
27. (Yezabeli; Sara; Hagari) alitimiza daraka katika drama ya mfano; aliwakilisha taifa la Israeli wa kimwili ambaye alikataliwa na Yehova. [ad uku. 39 fu. 1]
28. Katika Afrika ya magharibi, watu wengi walisikia mara ya kwanza ukweli kwa msaada wa hotuba za kibiblia zenye kuchochea za (Edwin Skinner; William Brown; Juan Muniz). [jv uku. 433 maf. 2-5]
29. Kwa kiburi, (Hamani; Hamathi; Hanuni) alijaribu kuteketeza Wayahudi; njama yake ilizuiliwa na malkia (Ruthu; Estheri; Debora). [ad uku. 637 fu. 5]
30. Yesu alikuja kuwa Masiya wakati wa (kuzaliwa kwake; ubatizo wake; ufufuo wake), ambao ulifanyika mwaka wa (2 K.W.W; 29 W.W; 33 W.W) [klSW uku. 65 fu. 12]
Patanisha habari zifuatazo na maandiko yanayolingana nayo: 1 Sam. 1:12-16; Mt. 4:8-10; Mt. 16:19; Yak. 1:13; 1 Yn. 5:19.
31. Mateso mengi yanayowasumbua wanadamu hayatokani na Mungu. [klSW uku. 71 fu. 3]
32. Wanafunzi wa kweli wa Yesu wanakataa kushiriki katika mambo ya siasa ya ulimwengu huu. [Usomaji wa Biblia; ona wSW96 5/1 uku. 12 fu. 9.]
33. Ujuzi kuhusu Ufalme wa Mungu ulifungua njia iongozayo mbinguni kwa Wayahudi, Wasamaria na Watu wa mataifa. [Usomaji wa Biblia; ona wSW91 3/15 uku. 5.]
34. Ikifikia kwamba wanatudharau, kwa ujumla litakuwa jambo la faida sana kwetu kuwa na mwelekeo wa unyenyekevu na kuitikia kwa heshima. [ad uku. 639 fu. 5]
35. Wakristo wanayo sababu nzuri ya kujitenga na ulimwengu. [klSW uku. 60 fu. 18]
S-97-SW Na. 291a 4/97