Watchtower—MAKTABA KU ENTERNETE
Watchtower
MAKTABA KU ENTERNETE
Kiswahili (Congo)
  • BIBLIA
  • VICHAPO
  • MIKUTANO
  • km 8/97 uku. 5-6
  • Kujikumbusha kwa Kuandika kwa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video juu ya habari yenye umechagua.

Pole, kulikuwa kosa fulani wakati video ilikuwa inajaribu kusoma.

  • Kujikumbusha kwa Kuandika kwa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1997
Huduma Yetu ya Ufalme—1997
km 8/97 uku. 5-6

Kujikumbusha kwa Kuandika kwa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Kujikumbusha vitabu vikiwa vyenye kufungwa kwa mambo yaliyozungumzwa kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma toka Mei 5 mpaka lile la Agosti 18, 1997. Jibu kwa kutumia karatasi tofauti kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Agizo: Wakati wa kujikumbusha, tumia tu Biblia. Mitajo inayotolewa kisha kila ulizo inatolewa ili kurahisisha utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu haionyeshwi kila mara kuhusu mitajo ya Mnara wa Mlinzi.]

Jibu Kweli au Si Kweli kisha sentensi zifuatazo:

1. Hizikia alifuata nyayo za baba yake, Ahazi, kwa kutia moyo ibada ya miungu ya uongo katika Yuda. [ad uku. 513]

2. Alama za siku za mwisho zinaonyeshwa tu katika Mathayo 24, Marko 13 na Luka 21. [klSW uku. 102 kisanduku]

3. Ulizo alilouliza Yohana Mbatizaji, linaloonyeshwa katika Luka 7:​19, linaonyesha ukosefu wa imani. [Usomaji wa Biblia; ona wSW87 1/1 uku. 16.]

4. Wakati wa Pasaka ya mwisho ambayo Yesu aliadhimisha pamoja na wanafunzi wake, Petro peke yake ndiye aliyemwambia: “Hakika mimi sitakukana kwa vyovyote.” [Usomaji wa Biblia]

5. Hakuna chochote katika Biblia kinachoonyesha kwamba mtume Petro alikuwa mwenye kuoa. [Usomaji wa Biblia]

6. Ufalme wa Kimasiya ambao Yesu alihubiri unakuja nafasi ya pili, ukiwa wenye kujitiisha chini ya enzi kuu ya Mungu ya ulimwengu wote mzima. [klSW uku. 91 fu. 4]

7. Herode Antipa ni mfalme ambaye alimkatisha kichwa Yohana Mbatizaji. [ad uku. 664]

8. Kwa kuwaambia Mafarisayo kwamba Ufalme wa Mungu ulikuwa katikati yao, Yesu alikuwa akijitambulisha kama Mfalme wa wakati ujao. (Luka 17:21) [klSW uku. 91 fu. 6]

9. Haiwezekani kwa kweli kufasiria kwa nini kitabu cha Luka kinatumia vokabilari (maneno) nyingi kuliko evanjeli nyingine zote tatu pamoja. [siSW uku. 187 fu. 2]

10. Wakati kazi ilipokuwa imepigwa marufuku katika Ulaya ya Mashariki, hakuna mwanamemba wowote wa Baraza linaloongoza aliyeweza kwenda katika sehemu hiyo ya ulimwengu. [jv uku. 506 fu. 1]

Jibu maulizo yafuatayo:

11. Ni filamu gani Sosaiti ilitoa katika 1954 ili kuwatolea watu sura ya tengenezo lionekanalo la Yehova na ukubwa walo? [jv uku. 480 fu. 3]

12. Namna gani wahubiri fulani wanashinda tatizo la kukuta watu na kuzungumza nao katika mahubiri? [jv uku. 516 maf. 2-4]

13. Kwa nini Yehova alimuamuru Eliya ‘apakae Hazaeli mafuta awe mfalme juu ya Suria?’ (1 Fal. 19:15) [ad uku. 643]

14. Yesu alikuwa akimaanisha nini aliposema: “Iweni na chumvi ndani yenu wenyewe, na dumisheni amani nyinyi kwa nyinyi.” (Marko 9:​50, TUM) [Usomaji wa Biblia; ona wF85 15/5 uku. 21 fu. 12.]

15. Ni somo gani lenye thamani tunaweza kupata kutokana na namna ambayo Yesu aliitikia kwa zawadi ya mjane maskini? (Marko 12:​42-44) [Usomaji wa Biblia; ona wSW87 12/1 uku. 29 fu. 6 mpaka uku. 30 fu. 1.]

16. Ni baadhi gani ya sifa za Petro zinaonekana katika mtindo wa kuandika wa Marko na hilo linaweza kufasiriwaje? [siSW uku. 182 maf. 5-6]

17. Ikiwa tunalinganisha Mathayo 6:​9, 10 na Luka 11:​2-4, kwa nini tunaweza kufikiri kwa usahihi kwamba haikuwa lazima kurudilia neno kwa neno sala ya Baba Yetu? [Usomaji wa Biblia; ona wSW90 5/15 uku. 16 fu. 6.]

18. Katika nini usomaji wa maandiko ya Biblia kama Luka 3:​1, 2 unajenga kutumaini kwetu katika kutegemeka kwa Biblia? [siSW uku. 188 fu. 7]

19. Ni maandiko gani ya Zaburi na Waebrania yanayoonyesha kwamba Yesu hangeanza kutawala papo hapo kisha kupanda kwake mbinguni? [klSW uku. 96 fu. 15]

20. Kwa kuwa Yesu hajakosa kamwe imani katika Mungu, kwa nini alilia: “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniachilia mbali?” (Marko 15:​34, TUM) [Usomaji wa Biblia; ona wSW87 6/15 uku. 31.]

Jaza nafasi zilizo wazi katika sentensi zifuatazo:

21. Ndoa ya Herode Antipa na Herodiasi ilikuwa ni muungano mara _________________________ na wa  _________________________ chini ya sheria ya wayahudi. [ad uku. 667]

22. Musa aliomba kwa shemegi yake, _________________________

kutumikia kama vile _________________________ kwa ajili ya Waisraeli wakati walipotoka Sinaï na kujielekeza kwenye _________________________ . [ad uku. 674]

23.  _________________________, mfalme wa Tiro, alimsaidia Sulemani wakati wa ujenzi wa hekalu kubwa kwa kumpa  _________________________ na sehemu ya  _________________________. [ad uku. 672]

24.  _________________________ imekuwa mojawapo ya nchi za kwanza-kwanza za Mashariki ya mbali kupokea wamishonari waliopewa mazoezi kwenye Gileadi wakati Harold King na Stanley Jones walipotumwa huko, katika 1947. [jv uku. 489 fu. 2]

25. Sibia na Light yalikuwa majina ya _________________________ zilizokuwa zikitumiwa na wamishonari ili kuhubiri katika Antilles. [jv uku. 463 fu. 1]

Onyesha majibu ya kweli katika habari zifuatazo:

26. Kwa kuwa kulikuwako uhitaji wa wamishonari, Shule (ya Huduma ya Kitheokrasi; ya Huduma ya Ufalme; ya Gileadi) ilifunguliwa katika (1939; 1943; 1946) ili kutimiza uhitaji huo. [jv uku. 458 fu. 2]

27. Kwenye karne ya kwanza (Alexenda; Diotrefesi; Himenayo) mwasi-imani, alikuwa akifundisha bila shaka kwamba ufufuo ulikuwa ni jambo la mfano na kwamba hakungekuwa na ufufuo wakati ujao. [ad uku. 688]

28. Mauaji ya kikundi ya vijana wanaume wote wa miaka miwili na kushuka chini kisha kuzaliwa kwa Yesu yaliamuriwa na (Herode Agripa I; Herode Antipa; Herode Mkuu) [ad ku. 663]

29. Wakati Yishmaëli alipokuwa akimchekelea Isaka, kulingana na Mwanzo 21:​8, 9, ulikuwa ndio mwanzo wa miaka (400; 430; 450) ya mateso ya Wayahudi, kipindi ambacho kingemalizika wakati Waisraeli wangekombolewa kutoka utumwani katika (Asiria; Babiloni; Misri) katika (537; 740; 1513) kabla ya wakati wetu. [ad uku. 724]

30. Kama inavyoripotiwa na (Mathayo 10; Mathayo 24; Luka 21), Yesu alitoa maagizo kamili kwa wale aliotuma kuhubiri. [siSW uku. 181 fu. 31]

Patanisha habari zifuatazo na maandiko yanayolingana nayo:

Marko 7:​20-23; 13:10; Luka 8:31; Matendo 12:​20-23; 17:11

31. Tungepaswa kwa haraka kuona kila uvutano mwovu au wenye kupotoka ambao ungeweza kuambukiza akili yetu na moyo wetu na kuutupilia mbali kabla haujazaa mizizi. [Usomaji wa Biblia; ona wSW89 11/1 uku. 14 fu. 16.]

32. Madaimoni (mashetani) watatupwa pamoja na Shetani katika kutokutenda kunakofanana na kifo muda wa “miaka elfu.” (Ufu. 20:3) [Usomaji wa Biblia]

33. Inafaa kutenda kwa haraka ili kwamba ushuhuda wa ulimwenguni pote uweze kutolewa katika wakati uliowekwa. [Usomaji wa Biblia]

34. Makumi ya maelfu ya watu walijifunza kusoma na kuandika pamoja na Mashahidi wa Yehova, jambo ambalo liliwawezesha kujifunza Biblia kibinafsi. [jv uku. 466 maf. 2-3]

35. Tungepaswa kuwa wenye busara kuhusu kujisifu, kwani kujitutumua kunamchukiza sana Mungu na pia wanadamu wengi. [ad uku. 665; ona pia wSW94 9/1 uku. 21.]

S-97-SW n° 292a 8/97

    Vichapo vya Swahili (Congo) (1996-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili (Congo)
    • Tumia Wengine
    • Préférences
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Kanuni za Matumizi
    • Kanuni za Kutunza Siri
    • Paramètres Kuhusu Kutunza Siri
    • JW.ORG
    • Ingia
    Tumia Wengine