Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yeremia 51
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Yeremia—Yaliyomo

      • Unabii dhidi ya Babiloni (1-64)

        • Babiloni litashindwa ghafla na Wamedi (8-12)

        • Kitabu chatupwa ndani ya Mto Efrati (59-64)

Yeremia 51:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Inaonekana hili ni jina la siri la Ukaldayo.

Marejeo

  • +Yer 50:9

Yeremia 51:2

Marejeo

  • +Yer 50:14, 29

Yeremia 51:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “asiukanyage.”

Marejeo

  • +Isa 13:17, 18; Yer 50:30

Yeremia 51:4

Marejeo

  • +Isa 13:15

Yeremia 51:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, nchi ya Wakaldayo.

Marejeo

  • +Zb 94:14; Isa 44:21; Yer 46:28; Zek 2:12

Yeremia 51:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nafsi yenu.”

Marejeo

  • +Yer 50:8; Zek 2:7; Ufu 18:4
  • +Yer 25:12, 14; 50:15

Yeremia 51:7

Marejeo

  • +Ufu 17:1, 2; 18:3
  • +Yer 25:15, 16

Yeremia 51:8

Marejeo

  • +Isa 21:9; 47:9; Ufu 14:8
  • +Ufu 18:2, 9

Yeremia 51:9

Marejeo

  • +Isa 13:14
  • +Ufu 18:4, 5

Yeremia 51:10

Marejeo

  • +Mik 7:9
  • +Yer 50:28

Yeremia 51:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “jazeni podo.”

Marejeo

  • +Yer 50:14
  • +Isa 13:17; 45:1

Yeremia 51:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nguzo ya ishara.”

Marejeo

  • +Isa 13:2
  • +Ufu 17:17

Yeremia 51:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kipimo.”

Marejeo

  • +Ufu 17:1, 15
  • +Isa 45:3; Yer 50:37
  • +Hab 2:9; Ufu 18:11, 12, 19

Yeremia 51:14

Marejeo

  • +Yer 50:15

Yeremia 51:15

Marejeo

  • +Zb 93:1; 104:24
  • +Zb 136:5; Met 3:19; Isa 40:22; Yer 10:12-16

Yeremia 51:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “huufanya mvuke upande.”

  • *

    Au labda, “malango.”

Marejeo

  • +Zb 135:7

Yeremia 51:17

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “sanamu yake ya kuyeyushwa.”

  • *

    Au “pumzi.”

Marejeo

  • +Isa 44:11
  • +Hab 2:19

Yeremia 51:18

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “ubatili.”

Marejeo

  • +Isa 41:29; Yer 14:22

Yeremia 51:19

Marejeo

  • +Kum 32:9
  • +Isa 47:4

Yeremia 51:24

Marejeo

  • +Zb 137:8

Yeremia 51:25

Marejeo

  • +Yer 50:31
  • +Yer 25:9

Yeremia 51:26

Marejeo

  • +Yer 50:13, 40; Ufu 18:21

Yeremia 51:27

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nguzo ya ishara.”

  • *

    Tnn., “Takaseni.”

Marejeo

  • +Isa 13:2; Yer 51:12
  • +Mwa 8:4
  • +Mwa 10:2, 3; Yer 50:41

Yeremia 51:28

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Takaseni.”

Marejeo

  • +Isa 13:17; Da 5:30, 31

Yeremia 51:29

Marejeo

  • +Isa 13:13, 19; Yer 50:13, 39, 40

Yeremia 51:30

Marejeo

  • +Isa 13:7
  • +Yer 50:37
  • +Zb 107:16; Isa 45:2

Yeremia 51:31

Marejeo

  • +Isa 47:11; Yer 50:24, 43

Yeremia 51:32

Marejeo

  • +Isa 44:27; Yer 50:38; Ufu 16:12

Yeremia 51:34

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Nebukadreza,” njia nyingine ya kuandika jina hili.

Marejeo

  • +2Nya 36:17, 18; Yer 50:17
  • +Yer 51:44

Yeremia 51:35

Marejeo

  • +Zb 137:8; Yer 50:29

Yeremia 51:36

Marejeo

  • +Yer 50:34
  • +Kum 32:35
  • +Isa 44:27; Yer 50:38

Yeremia 51:37

Marejeo

  • +Yer 25:12; 50:15
  • +Isa 13:19, 22
  • +Yer 50:13, 39

Yeremia 51:38

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “wanasimba wenye manyoya marefu shingoni.”

Yeremia 51:39

Marejeo

  • +Da 5:1, 4
  • +Yer 25:17, 27; 51:57

Yeremia 51:41

Maelezo ya Chini

  • *

    Inaonekana hili ni jina la siri la Babeli (Babiloni).

Marejeo

  • +Yer 25:17, 26
  • +Isa 13:19; Yer 49:25; Da 4:30

Yeremia 51:43

Marejeo

  • +Isa 13:1, 20; Yer 50:39

Yeremia 51:44

Marejeo

  • +Isa 46:1; Yer 50:2
  • +2Nya 36:7; Ezr 1:7; Yer 51:34; Da 1:1, 2
  • +Yer 51:58

Yeremia 51:45

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nafsi zenu.”

Marejeo

  • +Isa 48:20; Ufu 18:4
  • +Yer 51:6; Zek 2:7
  • +Isa 13:13

Yeremia 51:47

Marejeo

  • +Isa 13:15; Da 5:30

Yeremia 51:48

Marejeo

  • +Isa 44:23; 48:20; 49:13; Ufu 18:20
  • +Yer 50:3, 41

Yeremia 51:49

Marejeo

  • +Yer 50:17; 51:24

Yeremia 51:50

Marejeo

  • +Yer 50:8; Ufu 18:4
  • +Ezr 1:3; Zb 137:5

Yeremia 51:51

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “wageni.”

Marejeo

  • +Zb 79:1; Omb 1:10

Yeremia 51:52

Marejeo

  • +Isa 13:15

Yeremia 51:53

Marejeo

  • +Isa 14:13; Da 4:30
  • +Yer 50:10

Yeremia 51:54

Marejeo

  • +Isa 13:6
  • +Yer 50:22, 23

Yeremia 51:56

Marejeo

  • +Isa 21:2
  • +Yer 50:36
  • +Kum 32:35; Zb 94:1; Isa 34:8; Yer 50:29; Ufu 18:5
  • +Zb 137:8

Yeremia 51:57

Marejeo

  • +Yer 25:27
  • +Yer 51:39

Yeremia 51:58

Marejeo

  • +Yer 50:15; 51:44
  • +Hab 2:13

Yeremia 51:59

Marejeo

  • +Yer 32:12; 36:4; 45:1

Yeremia 51:62

Marejeo

  • +Isa 13:1, 20; 14:23; Yer 50:3, 39; 51:29, 37

Yeremia 51:64

Marejeo

  • +Ufu 18:21
  • +Yer 51:58

Jumla

Yer. 51:1Yer 50:9
Yer. 51:2Yer 50:14, 29
Yer. 51:3Isa 13:17, 18; Yer 50:30
Yer. 51:4Isa 13:15
Yer. 51:5Zb 94:14; Isa 44:21; Yer 46:28; Zek 2:12
Yer. 51:6Yer 50:8; Zek 2:7; Ufu 18:4
Yer. 51:6Yer 25:12, 14; 50:15
Yer. 51:7Ufu 17:1, 2; 18:3
Yer. 51:7Yer 25:15, 16
Yer. 51:8Isa 21:9; 47:9; Ufu 14:8
Yer. 51:8Ufu 18:2, 9
Yer. 51:9Isa 13:14
Yer. 51:9Ufu 18:4, 5
Yer. 51:10Mik 7:9
Yer. 51:10Yer 50:28
Yer. 51:11Yer 50:14
Yer. 51:11Isa 13:17; 45:1
Yer. 51:12Isa 13:2
Yer. 51:12Ufu 17:17
Yer. 51:13Ufu 17:1, 15
Yer. 51:13Isa 45:3; Yer 50:37
Yer. 51:13Hab 2:9; Ufu 18:11, 12, 19
Yer. 51:14Yer 50:15
Yer. 51:15Zb 93:1; 104:24
Yer. 51:15Zb 136:5; Met 3:19; Isa 40:22; Yer 10:12-16
Yer. 51:16Zb 135:7
Yer. 51:17Isa 44:11
Yer. 51:17Hab 2:19
Yer. 51:18Isa 41:29; Yer 14:22
Yer. 51:19Kum 32:9
Yer. 51:19Isa 47:4
Yer. 51:24Zb 137:8
Yer. 51:25Yer 50:31
Yer. 51:25Yer 25:9
Yer. 51:26Yer 50:13, 40; Ufu 18:21
Yer. 51:27Isa 13:2; Yer 51:12
Yer. 51:27Mwa 8:4
Yer. 51:27Mwa 10:2, 3; Yer 50:41
Yer. 51:28Isa 13:17; Da 5:30, 31
Yer. 51:29Isa 13:13, 19; Yer 50:13, 39, 40
Yer. 51:30Isa 13:7
Yer. 51:30Yer 50:37
Yer. 51:30Zb 107:16; Isa 45:2
Yer. 51:31Isa 47:11; Yer 50:24, 43
Yer. 51:32Isa 44:27; Yer 50:38; Ufu 16:12
Yer. 51:342Nya 36:17, 18; Yer 50:17
Yer. 51:34Yer 51:44
Yer. 51:35Zb 137:8; Yer 50:29
Yer. 51:36Yer 50:34
Yer. 51:36Kum 32:35
Yer. 51:36Isa 44:27; Yer 50:38
Yer. 51:37Yer 25:12; 50:15
Yer. 51:37Isa 13:19, 22
Yer. 51:37Yer 50:13, 39
Yer. 51:39Da 5:1, 4
Yer. 51:39Yer 25:17, 27; 51:57
Yer. 51:41Yer 25:17, 26
Yer. 51:41Isa 13:19; Yer 49:25; Da 4:30
Yer. 51:43Isa 13:1, 20; Yer 50:39
Yer. 51:44Isa 46:1; Yer 50:2
Yer. 51:442Nya 36:7; Ezr 1:7; Yer 51:34; Da 1:1, 2
Yer. 51:44Yer 51:58
Yer. 51:45Isa 48:20; Ufu 18:4
Yer. 51:45Yer 51:6; Zek 2:7
Yer. 51:45Isa 13:13
Yer. 51:47Isa 13:15; Da 5:30
Yer. 51:48Isa 44:23; 48:20; 49:13; Ufu 18:20
Yer. 51:48Yer 50:3, 41
Yer. 51:49Yer 50:17; 51:24
Yer. 51:50Yer 50:8; Ufu 18:4
Yer. 51:50Ezr 1:3; Zb 137:5
Yer. 51:51Zb 79:1; Omb 1:10
Yer. 51:52Isa 13:15
Yer. 51:53Isa 14:13; Da 4:30
Yer. 51:53Yer 50:10
Yer. 51:54Isa 13:6
Yer. 51:54Yer 50:22, 23
Yer. 51:56Isa 21:2
Yer. 51:56Yer 50:36
Yer. 51:56Kum 32:35; Zb 94:1; Isa 34:8; Yer 50:29; Ufu 18:5
Yer. 51:56Zb 137:8
Yer. 51:57Yer 25:27
Yer. 51:57Yer 51:39
Yer. 51:58Yer 50:15; 51:44
Yer. 51:58Hab 2:13
Yer. 51:59Yer 32:12; 36:4; 45:1
Yer. 51:62Isa 13:1, 20; 14:23; Yer 50:3, 39; 51:29, 37
Yer. 51:64Ufu 18:21
Yer. 51:64Yer 51:58
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
  • 30
  • 31
  • 32
  • 33
  • 34
  • 35
  • 36
  • 37
  • 38
  • 39
  • 40
  • 41
  • 42
  • 43
  • 44
  • 45
  • 46
  • 47
  • 48
  • 49
  • 50
  • 51
  • 52
  • 53
  • 54
  • 55
  • 56
  • 57
  • 58
  • 59
  • 60
  • 61
  • 62
  • 63
  • 64
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Yeremia 51:1-64

Yeremia

51 Yehova anasema hivi:

“Tazameni, ninaleta upepo unaoharibu

Dhidi ya Babiloni+ na dhidi ya wakaaji wa Leb-kamai.*

 2 Nitawatuma wapepetaji Babiloni,

Nao watampepeta na kuifanya nchi yake kuwa tupu;

Watamshambulia kutoka pande zote siku ya msiba.+

 3 Anayepiga mishale asiupinde* upinde wake.

Na yeyote asisimame akiwa amevaa koti lake la vita.

Msiwahurumie vijana wake.+

Angamizeni jeshi lake lote.

 4 Nao watauawa katika nchi ya Wakaldayo,

Wakiwa wamechomwa kwa silaha katika barabara zake.+

 5 Kwa maana Mungu wa Israeli na Yuda, Yehova wa majeshi, hajawaacha wakiwa wajane.+

Lakini nchi yao* imejaa hatia machoni pa Mtakatifu wa Israeli.

 6 Kimbieni kutoka Babiloni,

Kimbieni ili mwokoe uhai wenu.*+

Msiangamie kwa sababu ya kosa lake.

Kwa maana ni wakati wa kisasi cha Yehova.

Anamlipa kulingana na matendo yake.+

 7 Babiloni amekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Yehova;

Aliilewesha dunia yote.

Mataifa yamekunywa divai yake;+

Ndiyo sababu mataifa yameshikwa na wazimu.+

 8 Babiloni ameanguka ghafla, naye amevunjika.+

Mwombolezeeni!+

Leteni zeri kwa ajili ya maumivu yake; labda atapona.”

 9 “Tulijaribu kumponya Babiloni, lakini hakupona.

Mwacheni, twendeni kila mmoja kwenye nchi yake.+

Kwa maana hukumu yake imefika mbinguni;

Iko juu kama mawingu.+

10 Yehova ametutendea haki.+

Njooni, tusimulie katika Sayuni kazi ya Yehova Mungu wetu.”+

11 “Isugueni mishale;+ chukueni ngao za mviringo.*

Yehova ameichochea roho ya wafalme wa Wamedi,+

Kwa sababu anakusudia kuiangamiza Babiloni.

Kwa maana hiki ndicho kisasi cha Yehova, kisasi kwa ajili ya hekalu lake.

12 Inueni ishara*+ dhidi ya kuta za Babiloni.

Imarisheni ulinzi, wekeni walinzi.

Watayarisheni wale wanaovizia.

Kwa maana Yehova ametunga mbinu,

Naye atatekeleza alichoahidi dhidi ya wakaaji wa Babiloni.”+

13 “Ewe mwanamke unayekaa juu ya maji mengi,+

Mwenye hazina nyingi,+

Mwisho wako umefika, kikomo* chako cha kupata faida.+

14 Yehova wa majeshi ameapa kwa nafsi yake,

‘Nitakujaza wanaume wengi kama nzige,

Nao watapiga kelele za ushindi juu yako.’+

15 Yeye ndiye Muumba wa dunia kwa nguvu zake,

Yule aliyeiimarisha ardhi inayozaa kwa hekima yake+

Na aliyezitandaza mbingu kwa uelewaji wake.+

16 Anapofanya sauti yake isikike,

Maji yaliyo mbinguni huwa na msukosuko,

Naye huyafanya mawingu yapande* kutoka kwenye miisho ya dunia.

Hutengeneza radi* kwa ajili ya mvua,

Naye huutoa upepo katika maghala yake.+

17 Kila mtu anatenda bila kutumia akili na bila ujuzi.

Kila fundi wa chuma ataaibishwa kwa sababu ya sanamu ya kuchongwa;+

Kwa maana sanamu yake ya chuma* ni uwongo,

Nazo hazina roho* ndani yake.+

18 Sanamu hizo ni udanganyifu,*+ kazi ya mzaha.

Siku yao ya hukumu itakapofika, zitaangamia.

19 Fungu la Yakobo si kama vitu hivyo,

Kwa maana Yeye ndiye aliyeumba kila kitu,

Hata fimbo ya urithi wake.+

Yehova wa majeshi ndilo jina lake.”+

20 “Wewe ni rungu langu la vita, silaha ya vita,

Kwa maana nitakutumia kuyavunjavunja mataifa.

Nitakutumia kuziangamiza falme.

21 Nitakutumia kumvunjavunja farasi na mpandaji wake.

Nitakutumia kulivunjavunja gari la vita na mwendeshaji wake.

22 Nitakutumia kumvunjavunja mwanamume na mwanamke.

Nitakutumia kumvunjavunja mzee na mvulana.

Nitakutumia kumvunjavunja mwanamume na mwanamke kijana.

23 Nitakutumia kumvunjavunja mchungaji na mifugo yake.

Nitakutumia kumvunjavunja mkulima na kundi lake la wanyama.

Nitakutumia kuwavunjavunja magavana na watawala wasaidizi.

24 Nami nitamlipa Babiloni na wakaaji wote wa Ukaldayo

Kwa sababu ya uovu wote ambao wametenda huko Sayuni mbele ya macho yenu,”+ asema Yehova.

25 “Tazama, niko dhidi yako,+ ewe mlima wa uharibifu,” asema Yehova,

“Wewe unayeiharibu dunia yote.+

Nitaunyoosha mkono wangu dhidi yako na kukubingirisha kutoka kwenye majabali

Na kukufanya uwe mlima ulioteketezwa kabisa.”

26 “Watu hawatachukua kutoka kwako jiwe la pembeni wala jiwe la msingi,

Kwa sababu utabaki ukiwa milele,”+ asema Yehova.

27 “Inueni ishara* katika nchi.+

Pigeni pembe kati ya mataifa.

Wekeni* mataifa ya kumshambulia.

Iteni dhidi yake falme za Ararati,+ Mini, na Ashkenazi.+

Wekeni juu yake ofisa mwandikishaji.

Wafanyeni farasi waje kama nzige wenye miiba.

28 Wekeni* mataifa ya kumshambulia,

Wafalme wa Umedi,+ magavana wake na watawala wake wote wasaidizi

Na nchi zote wanazozitawala.

29 Nayo dunia itatetemeka na kutikisika,

Kwa maana mawazo ya Yehova dhidi ya Babiloni yatatekelezwa

Ili kuifanya nchi ya Babiloni kuwa kitu cha kutisha, bila mkaaji.+

30 Mashujaa wa Babiloni wameacha kupigana.

Wanaketi kwenye ngome zao.

Nguvu zao zimekwisha.+

Wamekuwa kama wanawake.+

Nyumba zake zimewashwa moto.

Makomeo yake yamevunjwa.+

31 Mleta habari mmoja anakimbia kukutana na mleta habari mwingine,

Na mjumbe mmoja kukutana na mjumbe mwingine,

Ili kumjulisha mfalme wa Babiloni kwamba jiji lake limetekwa kila upande,+

32 Kwamba vivuko vimetekwa,+

Kwamba mashua za mafunjo zimeteketezwa kwa moto,

Na kwamba wanajeshi wana hofu.”

33 Kwa maana Yehova wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi:

“Binti ya Babiloni ni kama uwanja wa kupuria.

Ni wakati wa kumkanyagia chini awe mgumu.

Hivi karibuni wakati wake wa mavuno utafika.”

34 “Mfalme Nebukadneza* wa Babiloni ameninyafua;+

Amenivuruga.

Ameniweka chini kama chombo kitupu.

Amenimeza kama nyoka mkubwa;+

Amelijaza tumbo lake kwa vitu vyangu vizuri.

Amenioshea mbali.

35 ‘Babiloni na alipizwe kwa sababu ya ukatili niliotendewa mimi na mwili wangu!’ asema mkaaji wa Sayuni.+

‘Na wakaaji wa Ukaldayo na walipizwe kwa sababu ya damu yangu!’ asema Yerusalemu.”

36 Kwa hiyo Yehova anasema hivi:

“Ninaitetea kesi yako,+

Nami nitakulipizia kisasi.+

Nitaikausha bahari yake na kuvikausha visima vyake.+

37 Na Babiloni atakuwa marundo ya mawe,+

Pango la mbwamwitu,+

Kitu cha kutisha na kitu cha kupigiwa mluzi,

Bila mkaaji.+

38 Wote pamoja watanguruma kama wanasimba.*

Watanguruma kama watoto wa simba.”

39 “Watakapokuwa wamesisimka, nitaandaa karamu yao na kuwalewesha,

Ili wafurahi;+

Kisha watalala usingizi wa kudumu,

Nao hawataamka kutoka katika usingizi huo,”+ asema Yehova.

40 “Nitawashusha chini kama wanakondoo kwenda machinjioni,

Kama kondoo dume pamoja na mbuzi.”

41 “Jinsi Sheshaki* alivyotekwa,+

Jinsi Sifa ya dunia yote ilivyokamatwa!+

Jinsi ambavyo Babiloni amekuwa kitu cha kutisha kati ya mataifa!

42 Bahari imekuja juu ya Babiloni.

Mawimbi yake mengi yamemfunika.

43 Majiji yake yamekuwa kitu cha kutisha, nchi isiyo na maji na jangwa.

Nchi ambayo hakuna mtu atakayeishi wala kupitia humo.+

44 Nitamkazia fikira Beli+ huko Babiloni,

Nami nitatoa kinywani mwake kile alichomeza.+

Mataifa hayatamiminika kwake tena.

Na ukuta wa Babiloni utaanguka.+

45 Tokeni kati yake, watu wangu!+

Kimbieni ili mwokoe uhai wenu*+ kutoka kwa hasira ya Yehova inayowaka!+

46 Msife moyo wala msiogope kwa sababu ya habari itakayosikiwa nchini.

Katika mwaka mmoja habari itakuja,

Na mwaka unaofuata habari nyingine,

Kuhusu ukatili nchini na kuhusu mtawala akimshambulia mtawala mwingine.

47 Kwa hiyo tazama! siku zinakuja

Nitakapozikazia fikira sanamu za kuchongwa za Babiloni.

Nchi yake yote itaaibishwa,

Na watu wake wote waliouawa wataanguka ndani yake.+

48 Mbingu na dunia na vyote vilivyomo

Vitapiga vigelegele vya shangwe kwa sababu ya Babiloni,+

Kwa maana waangamizaji watamvamia kutoka kaskazini,”+ asema Yehova.

49 “Babiloni hakusababisha tu kuuawa kwa Waisraeli walioanguka+

Bali pia huko Babiloni watu waliouawa wa dunia yote wameanguka.

50 Ninyi mnaoponyoka upanga, endeleeni kupiga mwendo, msisimame tuli!+

Mkumbukeni Yehova kutoka mbali,

Yerusalemu na aingie moyoni mwenu.”+

51 “Tumeaibishwa, kwa maana tumesikia dhihaka.

Nyuso zetu zimefunikwa kwa fedheha,

Kwa maana watu wa nchi ya kigeni* wameshambulia mahali patakatifu pa nyumba ya Yehova.”+

52 “Kwa hiyo tazameni! siku zinakuja,” asema Yehova,

“Nitakapozikazia fikira sanamu zake za kuchongwa,

Na katika nchi yake yote waliojeruhiwa watalia kwa maumivu.”+

53 “Hata Babiloni akipanda juu mbinguni,+

Hata akiimarisha ngome zake ndefu,

Watakaomwangamiza watakuja kutoka kwangu,”+ asema Yehova.

54 “Sikilizeni! Kuna kilio kikubwa kutoka Babiloni,+

Sauti ya msiba mkubwa kutoka nchi ya Wakaldayo,+

55 Kwa maana Yehova analiangamiza Babiloni,

Atainyamazisha sauti yake kubwa,

Na mawimbi yao yatavuma kama maji mengi.

Kelele ya sauti yao itasikika.

56 Kwa maana mwangamizaji ataishambulia Babiloni;+

Mashujaa wake watakamatwa,+

Pinde zao zitavunjwavunjwa,

Kwa maana Yehova ni Mungu wa kisasi.+

Bila shaka atalipa kisasi.+

57 Nitawalewesha wakuu wake na watu wake wenye hekima,+

Magavana wake na watawala wake wasaidizi na mashujaa wake,

Nao watalala usingizi wa kudumu,

Nao hawataamka kutoka katika usingizi huo,”+ asema Mfalme, ambaye jina lake ni Yehova wa majeshi.

58 Yehova wa majeshi anasema hivi:

“Ingawa ukuta wa Babiloni ni mpana, utabomolewa kabisa,+

Na ingawa malango yake ni marefu, yatawashwa moto.

Watu watafanya kazi ya bure;

Mataifa yatajichosha ili tu kuuchochea moto.”+

59 Hili ndilo neno ambalo nabii Yeremia alimwamuru Seraya mwana wa Neria+ mwana wa Mahseya alipoenda na Mfalme Sedekia wa Yuda huko Babiloni katika mwaka wa nne wa utawala wake; Seraya alikuwa msimamizi wa makao. 60 Yeremia aliandika katika kitabu kimoja msiba wote ambao ungepata Babiloni, maneno hayo yote yaliyoandikwa dhidi ya Babiloni. 61 Isitoshe, Yeremia akamwambia Seraya: “Utakapofika Babiloni na kuliona jiji hilo, lazima uyasome kwa sauti kubwa maneno haya yote. 62 Kisha useme, ‘Ee Yehova, umesema dhidi ya mahali hapa kwamba pataangamizwa na kubaki bila mkaaji, mwanadamu au mnyama, na kwamba patabaki ukiwa milele.’+ 63 Na utakapomaliza kukisoma kitabu hiki, utakifunga kwenye jiwe na kukitupa katikati ya Mto Efrati. 64 Kisha useme, ‘Hivi ndivyo Babiloni atakavyozama naye hatainuka tena kamwe+ kwa sababu ya msiba ambao ninamletea; nao watachoka.’”+

Maneno ya Yeremia yamefikia hapa.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki