Luka
19 Naye akaingia Yeriko na akawa akipita ndani. 2 Sasa hapa palikuwa na mwanamume aitwaye Zakayo kwa jina; naye alikuwa mkusanya-kodi-mkuu, na alikuwa tajiri. 3 Basi, alikuwa akitafuta sana kuona Yesu huyu alikuwa nani, lakini hangeweza kwa sababu ya umati, kwa sababu alikuwa mdogo kwa kimo. 4 Kwa hiyo akakimbia mbele kwenye mahali pa utangulio na kupanda mti mforsadi-tini kusudi amwone, kwa sababu alikuwa karibu kupitia njia hiyo. 5 Sasa Yesu alipofika mahali hapo, alitazama juu na kumwambia: “Zakayo, fanya haraka ushuke chini, kwa maana leo lazima mimi nikae katika nyumba yako.” 6 Ndipo akafanya haraka akashuka chini akampokea kwa mshangilio awe mgeni-mwalikwa wake. 7 Lakini walipoona hilo, wote wakaanza kunung’unika, wakisema: “Aliingia apate kukaa pamoja na mwanamume aliye mtenda-dhambi.” 8 Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana: “Tazama! Nusu ya mali zangu, Bwana, mimi ninawapa maskini, na chochote kile nilichonyang’anya yeyote kwa shtaka lisilo la kweli ninarudisha mara nne.” 9 Ndipo Yesu akamwambia: “Siku hii wokovu umekuja kwenye nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Abrahamu. 10 Kwa maana Mwana wa binadamu alikuja kutafuta sana na kuokoa kilichopotezwa.”
11 Walipokuwa wakisikiliza mambo hayo alisema kielezi kwa kuongezea, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu nao walikuwa wakiwazia kwamba ufalme wa Mungu ulikuwa ukielekea kujionyesha mara hiyo. 12 Kwa hiyo akasema: “Mtu fulani wa uzawa wa kikabaila alisafiri hadi nchi ya mbali ili ajipatie mamlaka ya kifalme kwa ajili yake mwenyewe na kurudi. 13 Akiita kumi kati ya watumwa wake aliwapa mina kumi na kuwaambia, ‘Fanyeni biashara hadi nije.’ 14 Lakini raia zake wakamchukia na kutuma baraza la mabalozi kumfuata, kusema, ‘Hatumtaki mtu huyu awe mfalme juu yetu.’
15 “Mwishowe aliporudi baada ya kupata mamlaka ya kifalme aliamuru waitwe kwake watumwa hao ambao alikuwa amewapa sarafu za fedha, kusudi ahakikishe kile walichokuwa wamepata faida kwa utendaji wa kibiashara. 16 Ndipo wa kwanza akajitokeza mwenyewe, akisema, ‘Bwana, mina yako ilipata faida ya mina kumi.’ 17 Kwa hiyo akamwambia, ‘Vema, mtumwa mwema! Kwa sababu katika jambo dogo sana umejithibitisha mwenyewe kuwa mwaminifu, uwe na mamlaka juu ya majiji kumi.’ 18 Sasa wa pili akaja, akisema, ‘Mina yako, Bwana, ilifanya mina tano.’ 19 Akamwambia huyu pia, ‘Wewe, pia, uwe na usimamizi juu ya majiji matano.’ 20 Lakini mwingine tofauti akaja, akisema, ‘Bwana, hii hapa mina yako, ambayo niliitunza ikiwa imehifadhiwa katika kitambaa. 21 Waona, nilikuhofu wewe, kwa sababu wewe ni mtu mgumu; wewe huchukua kile ambacho hukuweka nawe huvuna kile ambacho hukupanda.’ 22 Akamwambia, ‘Kutoka kwenye kinywa chako mwenyewe nakuhukumu, mtumwa mwovu. Ulijua, sivyo, kwamba mimi ni mtu mgumu, mwenye kuchukua kile ambacho sikuweka na kuvuna kile ambacho sikupanda? 23 Kwa sababu hiyo kwa nini hukutia sarafu zangu za fedha katika benki? Kisha niwasilipo ningalizichukua pamoja na faida.’
24 “Ndipo akawaambia wale wenye kusimama kando, ‘Chukueni hiyo mina kutoka kwake mmpe yeye aliye na mina kumi.’ 25 Lakini wao wakamwambia, ‘Bwana, yeye ana mina kumi!’— 26 ‘Mimi nawaambia nyinyi, Kwa kila mtu aliye nacho, atapewa zaidi; lakini kutoka kwa yule asiye nacho, hata kile alicho nacho kitaondolewa mbali. 27 Zaidi ya hilo, maadui wangu hawa ambao hawakunitaka niwe mfalme juu yao waleteni hapa mwachinje mbele yangu.’”
28 Kwa hiyo, alipokuwa amesema mambo hayo, alianza kwenda mbele, akipanda kwenda Yerusalemu. 29 Naye alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima uitwao Mlima wa Mizeituni, alituma wawili wa wanafunzi, 30 akisema: “Nendeni mwingie katika kijiji kilicho karibu yenu, na ndani yacho mkiisha kuingia mtakuta mwana-punda amefungwa, ambaye hakuna yeyote kati ya wanadamu aliyepata kuketi juu yake wakati wowote. Mfungueni mmlete. 31 Lakini mtu yeyote akiwauliza nyinyi, ‘Kwa nini mnamfungua?’ Lazima mseme kwa njia hii, ‘Bwana amhitaji.’” 32 Kwa hiyo wale waliotumwa wakaondoka wakakuta sawa na vile alivyowaambia. 33 Lakini walipokuwa wakimfungua mwana-punda wenye kummiliki wakawaambia: “Kwa nini mnafungua huyo mwana-punda?” 34 Wakasema: “Bwana amhitaji.” 35 Nao wakamwongoza kwa Yesu, nao wakatupa mavazi yao ya nje juu ya huyo mwana-punda na kumweka Yesu juu yake.
36 Alipokuwa akisonga mbele wakafuliza kutandaza mavazi yao ya nje barabarani. 37 Mara tu alipokaribia barabara ya kuteremkia Mlima wa Mizeituni umati wote wa wanafunzi ukaanza kushangilia na kusifu Mungu kwa sauti kubwa kuhusu kazi zote zenye nguvu ulizokuwa umeona, 38 ukisema: “Mbarikiwa ni Yule anayekuja akiwa ndiye Mfalme katika jina la Yehova! Amani mbinguni, na utukufu katika mahali palipoinuka juu zaidi sana!” 39 Hata hivyo, baadhi ya Mafarisayo kutoka kwenye umati wakamwambia: “Mwalimu, kemea wanafunzi wako.” 40 Lakini kwa kujibu akasema: “Mimi nawaambia nyinyi, Kama hawa wangekaa kimya, mawe yangepaaza kilio.”
41 Naye alipokaribia hapo, akalitazama jiji na kutoa machozi juu yalo, 42 akisema: “Kama wewe, naam, wewe, ungalikuwa umefahamu siku hii mambo yenye kuhusiana na amani—lakini sasa yamefichwa kutoka kwenye macho yako. 43 Kwa sababu siku zitakuja juu yako wakati maadui wako watakapojenga kukuzunguka wewe boma lenye miti iliyochongoka nao watakuzunguka na kukutaabisha kutoka kila upande, 44 nao watabwaga kwenye ardhi wewe na watoto wako walio ndani yako, nao hawataacha jiwe juu ya jiwe katika wewe, kwa sababu hukufahamu wakati wa kukaguliwa kwako.”
45 Naye akaingia katika hekalu na kuanza kuwafukuza nje wale waliokuwa wakiuza, 46 akiwaambia: “Imeandikwa, ‘Na nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,’ lakini nyinyi mliifanya pango la wapokonyaji.”
47 Zaidi ya hilo, yeye akawa akifundisha kila siku katika hekalu. Lakini makuhani wakuu na waandishi na walio wakubwa wa watu walikuwa wakitafuta kumwangamiza; 48 na bado hawakupata jambo lililo na matokeo walifanye, kwa maana watu wote walifuliza kushikamana sana naye ili wamsikie.