Luka
3 Mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwa Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa gavana wa Yudea, na Herode alipokuwa mtawala wa wilaya ya Galilaya, lakini Filipo ndugu yake alikuwa mtawala wa wilaya wa nchi ya Ituraya na Trakonitisi, na Lisaniasi alikuwa mtawala wa wilaya ya Abilene, 2 Siku za kuhani mkuu Anasi na za Kayafa, tangazo la Mungu likamjia Yohana mwana wa Zekaria nyikani.
3 Basi akaja kuingia katika nchi yote kuzunguka Yordani, akihubiri ubatizo katika ufananisho wa toba kwa msamaha wa dhambi, 4 kama vile imeandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii: “Sikilizeni! Mtu fulani anapaaza kilio nyikani, ‘Tayarisheni njia ya Yehova, nyinyi watu, fanyeni barabara zake ziwe nyoofu. 5 Kila mtaro lazima ujazwe, na kila mlima na kilima vifanywe tambarare, na mapindi lazima yawe njia zilizo nyoofu na mahali penye miparuzo njia zilizo laini; 6 na mwili wote utaona njia ya kuokoa ya Mungu.’”
7 Kwa hiyo akaanza kuambia umati wenye kujitokeza ili kubatizwa naye: “Nyinyi uzao wa nyoka-vipiri, ni nani ambaye amewadokezea nyinyi kuikimbia hasira ya kisasi inayokuja? 8 Basi tokezeni matunda yafaayo toba. Na msianze kusema ndani yenu wenyewe, ‘Sisi tuna baba yetu Abrahamu.’ Kwa maana nawaambia nyinyi kwamba Mungu ana nguvu za kuinulia Abrahamu watoto kutoka katika mawe haya. 9 Kwa kweli, tayari shoka limewekwa kwenye mzizi wa miti; kwa hiyo, kila mti usiotokeza matunda bora wapaswa kukatwa na kutupwa ndani ya moto.”
10 Na umati ukawa wamuuliza: “Basi, tutafanya nini?” 11 Kwa kujibu akawa akiwaambia: “Acheni mtu aliye na mavazi mawili ya ndani ashiriki pamoja na mtu ambaye hana hata moja, na acheni aliye na vitu vya kula afanye hivyohivyo.” 12 Lakini hata wakusanya-kodi wakaja ili kubatizwa, nao wakamwambia: “Mwalimu, tutafanya nini?” 13 Akawaambia: “Msidai kitu chochote zaidi kuliko kiwango cha kodi.” 14 Pia, wale walio katika utumishi wa kijeshi wakawa wakimuuliza: “Na sisi pia tutafanya nini?” Naye akawaambia: “Msisumbue mtu yeyote wala kushtaki mtu yeyote isivyo kweli, bali mtosheke na maposho yenu.”
15 Basi kwa kuwa watu walikuwa wakitarajia na wote walikuwa wakiwazawaza mioyoni mwao juu ya Yohana: “Je, labda yeye ndiye Kristo?” 16 Yohana alitoa jibu, akiwaambia wote: “Mimi, kwa upande wangu, nawabatiza nyinyi kwa maji; lakini mwenye nguvu zaidi kuliko mimi anakuja, ambaye gidamu ya makubazi yake mimi sistahili kufungua. Yeye atawabatiza nyinyi watu kwa roho takatifu na moto. 17 Sepetu yake ya kupepetea imo mkononi mwake ili kusafisha kabisa sakafu yake ya kupuria na kukusanya ngano ghalani mwake, lakini makapi atayachoma kabisa kwa moto usioweza kuzimwa.”
18 Kwa hiyo alitoa pia mahimizo mengine mengi yenye bidii na kuendelea kuwatangazia watu habari njema. 19 Lakini Herode mtawala wa wilaya, kwa kukaripiwa naye kuhusu Herodiasi mke wa ndugu yake na kuhusu vitendo viovu vyote alivyofanya Herode, 20 aliongeza hili pia kwa vitendo vyote hivyo: alimfungia Yohana gerezani.
21 Basi watu wote walipokuwa wamebatizwa, Yesu pia akabatizwa na, alipokuwa akisali, mbingu ilifunguliwa 22 na roho takatifu katika umbo la kiwiliwili kama njiwa ikateremka juu yake, na sauti ikaja kutoka mbinguni: “Wewe ni Mwana wangu, mpendwa; nimekukubali wewe.”
23 Zaidi ya hilo, Yesu mwenyewe, alipoanza kazi yake, alikuwa na umri wa karibu miaka thelathini, akiwa mwana, kama ilivyodhaniwa,
wa Yosefu,
mwana wa Heli,
24 mwana wa Mathati,
mwana wa Lawi,
mwana wa Melki,
mwana wa Yanai,
mwana wa Yosefu,
25 mwana wa Matathiasi,
mwana wa Amosi,
mwana wa Nahumu,
mwana wa Esli,
mwana wa Nagai,
26 mwana wa Maathi,
mwana wa Matathiasi,
mwana wa Semeini,
mwana wa Yoseki,
mwana wa Yoda,
27 mwana wa Yoanani,
mwana wa Resa,
mwana wa Zerubabeli,
mwana wa Shealtieli,
mwana wa Neri,
28 mwana wa Melki,
mwana wa Adi,
mwana wa Kosamu,
mwana wa Elmadamu,
mwana wa Eri,
29 mwana wa Yesu,
mwana wa Eliezeri,
mwana wa Yorimu,
mwana wa Mathati,
mwana wa Lawi,
30 mwana wa Simioni,
mwana wa Yudasi,
mwana wa Yosefu,
mwana wa Yonamu,
mwana wa Eliakimu,
31 mwana wa Melea,
mwana wa Mena,
mwana wa Matatha,
mwana wa Nathani,
mwana wa Daudi,
32 mwana wa Yese,
mwana wa Obedi,
mwana wa Boazi,
mwana wa Salmoni,
mwana wa Nashoni,
33 mwana wa Aminadabu,
mwana wa Arni,
mwana wa Hezroni,
mwana wa Perezi,
mwana wa Yuda,
34 mwana wa Yakobo,
mwana wa Isaka,
mwana wa Abrahamu,
mwana wa Tera,
mwana wa Nahori,
35 mwana wa Serugi,
mwana wa Reu,
mwana wa Pelegi,
mwana wa Eberi,
mwana wa Shela,
36 mwana wa Kainani,
mwana wa Arpakshadi,
mwana wa Shemu,
mwana wa Noa,
mwana wa Lameki,
37 mwana wa Methusela,
mwana wa Enoki,
mwana wa Yaredi,
mwana wa Mahalaleeli,
mwana wa Kainani,
38 mwana wa Enoshi,
mwana wa Sethi,
mwana wa Adamu,
mwana wa Mungu.