1 Wathesalonike
3 Kwa sababu hiyo, wakati sisi hatungeweza kuhimili hilo tena, tuliona vema kuachwa peke yetu katika Athene; 2 nasi tukamtuma Timotheo, ndugu yetu na mhudumu wa Mungu katika habari njema juu ya Kristo, kusudi awafanye nyinyi imara na kuwafariji kwa niaba ya imani yenu, 3 kwamba yeyote asipate kuyumbishwa na dhiki hizi. Kwa maana nyinyi wenyewe mwajua tumewekewa jambo hilihili. 4 Kwa kweli, pia, wakati tulipokuwa pamoja nanyi, tulikuwa na kawaida ya kuwaambia nyinyi kimbele kwamba tulikusudiwa kupatwa na dhiki, kama vile imetukia pia na kama mjuavyo. 5 Hiyo ndiyo sababu, kwa kweli, wakati mimi singeweza kuhimili hilo tena, nilituma mtu ili nijue juu ya uaminifu wenu, kama labda kwa njia fulani yule Mshawishi angekuwa amewashawishi nyinyi, na kazi yetu ya jasho ingekuwa imetokea kuwa bure.
6 Lakini Timotheo amekuja sasa hivi kutoka kwenu na kutupa sisi habari njema juu ya uaminifu na upendo wenu, na kwamba mwaendelea kuwa na ukumbuko mwema juu yetu sikuzote, mkitamani sana kutuona kwa njia ileile, kwa kweli, kama vile sisi pia tutamanivyo kuwaona nyinyi. 7 Hiyo ndiyo sababu, akina ndugu, tumefarijiwa juu yenu nyinyi katika uhitaji wetu wote na dhiki kupitia uaminifu mwonyeshao, 8 kwa sababu sasa twaishi ikiwa nyinyi mwasimama imara katika Bwana. 9 Kwa maana ni utoaji-shukrani gani tuwezao kutoa kwa Mungu kuhusu nyinyi kuwa malipo ya shangwe yote ambayo sisi tunashangilia kwayo kwa sababu yenu mbele ya Mungu wetu, 10 huku usiku na mchana tukiomba dua ambazo ni zaidi kuliko zile za kawaida ili tuone nyuso zenu na kuboresha mambo yanayokosekana juu ya imani yenu?
11 Sasa Mungu wetu na Baba mwenyewe na Bwana wetu Yesu na wapate kuelekeza kwa ufanisi njia yetu ya kuwajia nyinyi. 12 Zaidi ya hayo, Bwana na asababishe nyinyi mwongezeke, ndiyo, awafanye nyinyi mzidi, katika upendo kwa mtu na mwenzake na kwa wote, kama vile sisi pia tuwafanyiavyo nyinyi; 13 kwa madhumuni ya kwamba apate kufanya mioyo yenu iwe imara, isiyolaumika katika utakatifu mbele ya Mungu wetu na Baba kwenye kuwapo kwa Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.