1 Wathesalonike
2 Kwa hakika, nyinyi wenyewe mwajua, akina ndugu, jinsi ziara yetu kwenu haikuwa bila matokeo, 2 bali jinsi, baada ya sisi kuwa tumeteseka kwanza na kutendwa kwa ufidhuli (kama vile nyinyi mjuavyo) katika Filipi, tulijipa ujasiri kwa njia ya Mungu wetu kusema nanyi habari njema ya Mungu kwa kushindana sana. 3 Kwa maana himizo lenye bidii ambalo sisi twatoa halitokani na kosa au kutokana na ukosefu wa usafi au na udanganyi, 4 bali, kama vile tumethibitishwa na Mungu kuwa twafaa kukabidhiwa habari njema, ndivyo sisi tusemavyo, kama wenye kupendeza, si wanadamu, bali Mungu, afanyaye ithibati ya mioyo yetu.
5 Kwa kweli, hakuna wakati wowote ambao sisi tumetokea ama na usemi wa kurai, (kama vile nyinyi mjuavyo) ama na sura isiyo ya kweli kwa ajili ya tamaa, Mungu ni shahidi! 6 Wala hatujawa tukitafuta sana utukufu kutoka kwa wanadamu, la, ama kutoka kwenu nyinyi au kutoka kwa wengine, ingawa tungeweza kuwa mzigo ulemeao wenye gharama tukiwa mitume wa Kristo. 7 Kinyume cha hilo, tulipata kuwa waanana katikati yenu, kama wakati mama mwenye kunyonyesha atunzavyo sana watoto wake mwenyewe. 8 Kwa hiyo, tukiwa na shauku nyororo kwa ajili yenu, tulipendezwa vema kuwapa nyinyi, si habari njema ya Mungu tu, bali pia nafsi zetu wenyewe, kwa sababu mlipata kuwa wapendwa kwetu.
9 Hakika mwazingatia akilini, akina ndugu, kazi yetu ya jasho na kumenyeka. Ilikuwa kwa kufanya kazi usiku na mchana, ili kutoweka mzigo ulemeao wenye gharama juu ya yeyote kati yenu, kwamba sisi tuliwahubiri nyinyi habari njema ya Mungu. 10 Nyinyi ni mashahidi, na Mungu pia, juu ya jinsi sisi tulivyothibitika kuwa waaminifu-washikamanifu na waadilifu na wasiolaumika kwenu nyinyi waamini. 11 Kwa upatano na hilo mwajua vema jinsi, kama vile baba afanyiavyo watoto wake, tulifuliza kuhimiza kwa bidii kila mmoja wenu, na kufariji na kuwatolea nyinyi ushahidi, 12 kwa madhumuni ya kwamba mwendelee kutembea kwa ustahili wa Mungu anayewaita nyinyi kwenye ufalme na utukufu wake.
13 Kwa kweli, hiyo ndiyo sababu sisi twamshukuru Mungu pia bila kukoma, kwa sababu nyinyi mlipopokea neno la Mungu, ambalo mlilisikia kutoka kwetu, mlilikubali, si kama neno la wanadamu, bali, kama vile lilivyo kwa kweli, kama neno la Mungu, ambalo pia lafanya kazi katika nyinyi waamini. 14 Kwa maana nyinyi mlipata kuwa waigaji, akina ndugu, wa makutaniko ya Mungu yaliyo katika Yudea katika muungano na Kristo Yesu, kwa sababu nyinyi pia mlianza kuteseka mikononi mwa wananchi wenzenu wenyewe mambo yaleyale kama yale ambayo wao pia wanateseka mikononi mwa Wayahudi, 15 walioua hata Bwana Yesu na manabii na kutunyanyasa sisi. Zaidi ya hilo, wao hawampendezi Mungu, bali wako dhidi ya masilahi ya wanadamu wote, 16 wajaribupo kutuzuia tusiseme na watu wa mataifa ili hao wapate kuokolewa, tokeo likiwa kwamba sikuzote wao hujaza kabisa kipimo cha dhambi zao. Lakini hasira yake ya kisasi hatimaye imekuja juu yao.
17 Kwa habari yetu wenyewe, akina ndugu, tulipoachwa ukiwa bila nyinyi kwa wakati mfupi tu, kwa uso, si katika moyo, tulijitahidi zaidi sana kuliko ilivyo kawaida ili kuona nyuso zenu tukiwa na tamaa kubwa. 18 Kwa sababu hiyo tulitaka kuwajia nyinyi, ndiyo, mimi Paulo, mara moja na pia mara ya pili, lakini Shetani akakatiza pito letu. 19 Kwa maana ni nini tumaini letu au shangwe au taji la mchachawo—kwani, je, kwa kweli si nyinyi?—mbele ya Bwana wetu Yesu kwenye kuwapo kwake? 20 Nyinyi hakika ni utukufu na shangwe yetu.