1 Wathesalonike
Ya Kwanza kwa Wathesalonike
1 Paulo na Silvano na Timotheo kwa kutaniko la Wathesalonike katika muungano na Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo:
Na mwe na fadhili isiyostahiliwa na amani.
2 Sikuzote twamshukuru Mungu tutajapo kuhusu nyinyi nyote katika sala zetu, 3 kwa maana bila kukoma twazingatia akilini kazi yenu ya uaminifu na kazi yenu ya jasho yenye upendo na uvumilivu wenu kwa sababu ya tumaini lenu katika Bwana wetu Yesu Kristo mbele ya Mungu wetu na Baba. 4 Kwa maana twajua, akina ndugu mliopendwa na Mungu, kuchaguliwa kwenu naye, 5 kwa sababu habari njema tuhubiriyo haikutokea miongoni mwenu kwa usemi pekee bali pia kwa nguvu na kwa roho takatifu na usadikisho wenye nguvu, kama vile nyinyi mjuavyo ni watu wa namna gani sisi tulipata kuwa kwenu kwa ajili yenu; 6 nanyi mkawa waigaji wetu na wa Bwana, kwa vile mlilipokea neno chini ya dhiki nyingi pamoja na shangwe ya roho takatifu, 7 hivi kwamba nyinyi mlipata kuwa kielelezo kwa waamini wote katika Makedonia na katika Akaya.
8 Uhakika ni kwamba, si kwamba neno la Yehova limevuma tu kutoka kwenu nyinyi katika Makedonia na Akaya, bali pia katika kila mahali imani yenu kuelekea Mungu imesambaa kotekote, hivi kwamba hatuhitaji kusema lolote. 9 Kwa maana wao wenyewe wanafuliza kuripoti juu ya jinsi sisi tulivyoingia kwanza miongoni mwenu na jinsi nyinyi mlivyomgeukia Mungu kutoka kwenye sanamu zenu ili mtumikie kama watumwa Mungu aliye hai na wa kweli, 10 na kungoja Mwana wake kutoka kwenye mbingu, ambaye yeye alifufua kutoka kwa wafu, yaani, Yesu, atukomboaye sisi kutoka kwenye hasira ya kisasi inayokuja.