29 Naye akamtundika mfalme wa Ai+ juu ya mti mpaka jioni;+ na jua lilipokaribia kutua, Yoshua akatoa amri nao wakachukua maiti yake+ kutoka mtini na kuitupa kwenye mwingilio wa lango la jiji nao wakaweka rundo kubwa la mawe juu yake, mpaka leo hii.
27 Na ikawa kwamba Yoshua akatoa amri wakati wa kutua kwa jua, nao wakawashusha kutoka juu ya miti+ hiyo na kuwatupa ndani ya pango ambamo walikuwa wamejificha. Kisha wakaweka mawe makubwa katika kinywa cha pango hilo—mpaka leo hii.
17 Mwishowe wakamchukua Absalomu, wakamtupa msituni ndani ya shimo kubwa, wakarundika juu yake fungu kubwa sana la mawe.+ Lakini Israeli wote wakakimbia, kila mtu akaenda nyumbani kwake.