20 Sasa yeye alitaka kupigana na watu wa Tiro na wa Sidoni. Kwa hiyo wakamjia kwa umoja na, baada ya kumshawishi Blasto, aliyekuwa msimamizi wa chumba cha kulala cha mfalme, wakaanza kutoa ombi la kutaka amani, kwa sababu nchi yao iligawiwa chakula+ kutoka katika kile cha mfalme.